Wednesday, February 3, 2016

SERIKALI YACHUKUA SAMPULI ZA MAJI MGODI NORTH MARA- Chanzo Gazeti la Nipashe la 02/02/2016


Serikali imewaagiza wataalamu wa upimaji wa kemikali wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na wale wa SGS katika mgodi wa North Mara, kuchukua sampuli ya maji yanayo lalamikiwa na wananchi wa Nyamongo kuwa yana kemikali zenye sumu na kuwa sababishia madhara.

Timu hiyo ya wataalamu kutoka mashirika hayo, imepewa jukumu hilo kutokana na majibu ya ‘mkanganyo’ aliyopewa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhanga Mpina, baada ya kutembelea mgodi huo wiki mbili zilizopita.

“Serikali imeamua kuwa chukua wataalamu hawa na Mkemia Mkuu wa serikali ili wayapime maji yaliyo chukuliwa sehemu yenye bwawa la kutunzia maji machafu, kwani inadaiwa yanapo tiririka nje ya mgodi huwa letea madhara wananchi”, alisema Mpina.

Aidha mpina aliwataka wananchi wawe na Imani na wataalamu hao kwa kazi watakayo fanya kutokana na serikali kuamua kuliangalia tatizo hilo ilikuhakikisha wananchi wake wanaishi kwenye mazingira salama.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia uchukuaji wa sampuli ya maji hayo, walimuomba Mpina kuhakikisha kuwa haufanyiki mchezo mchafu katika upimaji kwani wao walisha chukua maji hayo yanayo wadhuru na kuyapeleka Nairobi nchini Kenya kwa vipimo, yaka bainika yana kemikali za sumu.

Naye Afisa wa Uhakiki wa TBS, Julieth Elibariki, alisema kinachotakiwa kupimwa ni maji na matokeo ya vipimo vine vya kitaalamu vinavyo julikana ‘micrology chemical paramenters, ‘organic compounds na contaminats’ huku matokeo ya vipimo hivyo yatachukua siku tano hadi saba ilikujulikana kama yana kemikali za sumu au vinginevyo.
 
KUMBUKUMBU YA TUKIO KAMA HILO
Siku ya Ijumaa tarehe 25 mwezi Aprili 2011, blog yetu iliwahi kutoa taarifa za baadhi ya wananchi wa Nyamongo ambako mgodi wa North Mara unaendesha shughuli zake, kuwa walipata madhara kutokana na maji yanayo tiririka kutoka mgodini kudaiwa kuwa na sumu.
Picha hapo chini zinaonesha baadhi ya wananchi walio athiriwa na maji hayo.
 
 

 
Pia jamii isisahau hata kidogo kile kilichotokea mwaka 2009, ambapo kemicali-sumu aina ya CYANIDE ilivuja na kuchanganyikana na maji yamto THIGITE, mto unaotumiwa na wanakijiji wa Nyamongo kama chanzo kikuu cha maji ya matumizi ya kila siku. Kutokana na tukio hilo, inakadiriwa watu wapatao Arobaini (40) walipoteza maisha, mamia wakiachwa na ulemavu wa kudumu na mifugo zaidi ya Mia Tano (500) ilikufa kutokana na kutumia maji yaliyochanganyikana na kemikali hiyo yenye sumu

 
 

 

No comments:

Post a Comment