Tuesday, January 4, 2011

KUFANYA KAZI YA KUJITOLEA NA CHAMA CHA WANASHERIA WATETEZI WA MAZINGIRA


Na, Evelyn Sanga
LEAT

Majina yetu ni Evelina Sanga na Baraka Saiteu tumekuwa tukifanya kazi za kujitolea katika asasi isiyo ya serikali inayojihusisha na Maswala ya mazingira na haki za binadamuinayojulikana kama . Chama cha wanasheria watetezi wa mazingira (LEAT) chini ya mradi wa  YETs unaodhaminiwa na World wide for Funds, katika mradi wa YETs tumeweza kupata ujuzi  mbalimbali kama vile kufudisha kuhusu mazingira kwenye ngazi ya jamii,maswala ya utunzaji wa mazingira, kusimamia miradi nk.

Katika kipindi chote tulichokuwa LEAT pia tuliweza kujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na mazingira na rasilimali zote ,kupata bahati ya kufanya kazi ya kujitolea  na LEAT kumetuongezea ujuzi katika kutoa elimu  ya Mazingira, na pia kutoa msaada wa Sheria unao husiana na Mazingira, Ardhi, na mengineyo, pia tumejifunza mambo yanayohusu haki za binadamu kwa ujumla wake.

KAZI TULIZOKUWA TUKIFANYA KATIKA KIPINDI CHA KUJITOLEA
TULIWAJIBIKA KUFANYA KAZI ZIFUATAZO
  • Kuelimisha / kutoa mafunzo  kuhusu maswala ya mazingira
  • Kutoa msaada wa kisheria kwenye jamii za kitanzania
  • Kufanya utafiti wa mazingira  na rasilimali katika maeneo mbalimbali.


Evelina Sanga (Katikati) na Baraka Saiteu (kushoto) wakiwa kwenye utafiti mdogo kuhusu mazingira maeneo ya Kihonda nje kidogo na Manispaa ya Morogoro 

FAIDA TULIZOZIPATA KUTOKANA NA KAZI TULIZO WAJIBIKA KUZIFANYA

Tumeweza kupanua uwigo wetu wa ufahamu kuhusu mazingira, mbali na hapo pia tumeweza kujiongezea  ujuzi katika shughuli zinazo husiana kufanya utafiti hasa katika sekta ya mazingira napia kusaidia jamii ya kitanzania katika maswala mbalimbali ya sheria.
Faida nyingine ni kupata fulsa ya kujua matatizo gani yanayowakabili watanzania na njia gani mbadala ya kupunguza matatizo hayo kama sio kutokomeza kabisa.

CHANGAMOTO TULIZO ZIPATA

Ni ukweli kwamba kila penye faida wakati mwingine hakukosi hasara, tulikabiliwa na changamoto japo si kwa ukubwa sana, changamoto hizo zilitokana na kazi tulizokuwa tukifanya mfano mzuri tulipokuwa tunatoa msaada wa sheria baadhi ya jamii tulizowafikia walikuwa wakitaka pesa kitu ambaho kilituwia vigumu sana katika utendaji wa kazi. 

Changamoto nyingine tuliyopata ni wakati tunatoa mafunzo kuhusu mazingira baadhi ya jamii tulizowafikia walikuwa wakitaka pesa zaidi ya zile tulizowajibika kuwapa kwa madai haziwatoshi,hicho pia kilikuwa kikwazo kwani ilichangia kupoteza uwepo na umakini katika kusikiliza mafundisho hivyo kukwamisha malengo ya kutoa mafundisho.

HITIMISHO

Tunapenda kutanguliza shukrani zetu za dhati kwa Chama cha wanasheria watetezi wa mazingira (LEAT) kwa Muda wote tulioweza kufanya kazi nao, tumeweza kuongeza ujuzi wetu katika utendaji wa kazi kitu ambacho ni Faida kubwa katika soko la ajira.
Mwisho kabisa tunapenda kuwaambia wananchi kuwa asasi ya LEAT inafanya kazi bila upendeleo hivyo wananchi wenye matatizo yahusuyo mazingira  mnakaribishwa.