Kuhusu LEAT

Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira (LEAT)ni asasi ya kwanza na ya kipekee inayojishughulisha na utetezi wa umma katika masuala ya yanayohusu mazingira, sheria za mazingira na maliasili Tanzania. Iliundwa mwaka 1994 na kusajiliwa 1995. Dira yake ni kuhakikisha kuwepo kwa uhifadhi na ulinzi mahiri na endelevu wa maliasili na mazingira Tanzania.

LEAT inafanya utafiti wa Sera na Sheria, utetezi na ushawishi, kuijengea jamii uwezo katika masuala ya sheria za mazingira na maliasili, inatoa msaada wa kisheria kwa masuala ya mazingira na maliasili.

Wanachama wa LEAT, kwa kiasi kikubwa ni Wanasheria waliobobea na wanaojihusisha na masuala ya uhifadhi endelevu wa mazingira na utawala wa kidemokrasia Tanzania.