HABARI KATIKA PICHA

MATUKIO MBALI MBALI YA MRADI WA USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA USIMAMIZI WA MALIASILI-IRINGA NA MUFINDI

Yafuatayo ni matukio mbali mbali ya mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili unaotekelezwa katika wilaya za Iringa vijijini na Mufindi mkoani Iringa. Mradi huu umefadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Mendeleo la Marekani, (USAID)-Tanzania.
Wilaya hizo zilichaguliwa kwa sababu zina maliasili za misitu na wanyamapori. Katika utekelezaji wa mradi huu LEAT inatoa mafunzo ya Usimamizi wa Maliasili pamoja na Ufuatilaiaji Uwajibikaji Jamii, ilikuiwezesha jamii kuwabana viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia maliasili za nchi.
 
Kulia ni Afisa Nyuki Wilaya ya Mufindi, Hamis Hassan akitoa maelekezo ya ufugaji nyuki kwa vikundi vya ufugaji nyuki wilayani Mufindi
 
 
Kushoto ni Afisa Nyuki wilaya ya Mufindi, Hamis Hassan na Kulia ni Mkurugenzi wa Asasi ya ASH-TECH, Erasto Mazera wakiwaonesha washiriki wa mafunzo, aina ya mzinga wa kufugia nyuki, mizinga hiyo ilitolewa bure na LEAT kwa kila mshiriki wa mafunzo ya ufugaji nyuki.
 
Baadhi ya washiriki wakifuatilia  mafunzo ya ufugaji nyuki wilayani Mufindi
 
 
Wafanyakazi wa LEAT pamoja na wadau kutoka Asasi za Kiraia wakati wa mkutano wa kupitia Mwongozo wa Mafunzo ya Ufugaji Nyuki. Kutoka kushoto ni Afisa Mradi wa LEAT Jamal Juma, Afisa Nyuki Mstaafu bwana Kahatano, Afisa Mradi wa LEAT Hanna Lupembe na bwana Simon Komba kutoka Asasi ya MJUMIKK

 Wadau wakijadili mapitio ya Mwongozo wa Mafunzo ya Ufugaji Nyuki, Mufindi Iringa.
Mkurugenzi wa Asasi ya ASH-TECH Erasto Mazera akiwasilisha matokeo ya utafiti wa ufugaji nyuki wa Asasi yake, wakati wa mapitio ya Mwongozo wa Mafunzo ya Ufugaji nyuki
 
Baadhi ya Wanatimu ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii kwa wilaya ya Iringa vijijini. Timu hiyo inaundwa na kamati za vijiji za Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii pamoja na maofisa wa serikali. Kazi ya timu hiyo ni kufuatilia na kutathmini uwajibikaji wa viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia maliasili pamoja na utoaji wa huduma mbali mbali za kijamii.

Katika picha ni baadhi ya Timu ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii wakipitia bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini

Maofisa Mradi wa LEAT Musa Msanizu na Hanna Lupembe wakipitia bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini, wakati wa vikao vya Timu za Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii, vilivyofanyika katika hoteli ya Rutheran, Iringa mjini.
 

ZIARA

 
 
Afisa Mwakilishi wa Makubaliano wa USAID, Mikala Laurdisen alipotembelea maeneo ya mradi. Hapo alikuwa katika kijiji cha Kiwere wilaya ya Iringa vijijini 
 
Kutoka kushoto ni Afisa Misitu wa wilaya ya Iringa vijijini bwana Mshana, Mtendaji wa kijiji cha Kiwere, Afisa Ufuatiliaji an Tathmini wa USAID bwana Charles, Mkurugenzi Mtendaji wa LEAT Dr. Nshala na Afisa Mwakilishi wa Makubaliano kutoka USAID, Mikal Laurdisen, katika ofisi ya kijiji cah Kiwere.
 
 
 

UTEKELEZAJI WA SHUGHULI MBALIMBALI KATIKA PICHA


Afisa Wanyamapori wa Morogoro akifafanua jambo katika Mafunzo yaliyoandaliwa na LEAT kwa Vijiji wanchama wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya WAMI MBIKI   



Mazingira magumu ya Uchimbaji Mdogo katika Machimbi ya Winza wilayani Mpwapwa



Washiriki wa Mafunzo ya Elimu ya Sheria za Rasilimali wilayani Karatu Arusha,

Mwezeshaji wa Masuala ya Mandeleo na Misitu akiwasilisha katika Mafunzo juu ya MKUHUMI na Malengo ya Milenia yaliyoandaliwa na LEAT wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Baadhi ya Washiriki katika Moja ya Semina wakifanya kazi za makundi kwa umakini mkubwa.

Wakufunzi na Wanafunzi wa Mazingira wa program ya YET inayosiendeshwa na WWF na LEAT ikiwa ni mwanachama.




Mwanasheria wa LEAT akifundisha kuhusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

1 comment: