Wednesday, February 24, 2016

Kutana na Salome Choga Mwanamke aliye dhamiria kuongeza kipato kupitia Mradi wa Ufugaji Nyuki


Salome Choga wakati wa mahojiano katika msitu wa kijiji cha Lugoda Lutali, Mufindi, Iringa


Salome Choga ni Mjumbe wa Kamati ya Maliasili ya kijiji cha Lugoda Lutali, wilayani Mufindi, mkoani Iringa. Kijiji hicho ni kati ya vijiji 32 vilivyofikiwa na mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili. Mradi huo unaratibiwa na Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa vitendo, (LEAT), kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani, (USAID).

Katika kipindi chote cha maisha yake, Salome amekuwa akitegemea biashara ndogondogo pamoja na kilimo alicho dai kuwa hakina tija sana, kwakuwa mapato hayakidhi mahitaji ya familia yake. Ana watoto wawili mmoja ana umri wa miaka kumi na nne na mwingine ana miaka kumi wote wanasoma katika shule ya msingi Lugoda Lutali. Kwa muda mrefu Salome ndiye mtafutaji wa kipato kwaajili ya familia baada ya mume wake kuondoka na kuishi mbali na familia.

Salome alipongeza Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT) kwa kuleta mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, uliofadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). “Mradi huu unaleta tija katika jamii kwani licha ya kuwa unafundisha na kuhamisisha jamii kulinda na kusimamia maliasili pia wametuletea mradi wa ufugaji nyuki kama njia mbadala ya mapato, ilikupunguza utegemezi wa mapato kwa kuuza rasilimali zilizopo katika misitu”, alisema.

Ingawa hakushiriki katika mafunzo ya ufugaji nyuki anatarajia kushiriki katika awamu ijayo. Katika kipindi chote cha maisha yake amekuwa akitegemea biashara ndogondogo pamoja na kilimo katika kujipatia mapato ya kuendesha maisha ya familia yake. Alieleza kuwa yeye ni mama wa watoto wawili na ndiye mlezi pekee wa watoto hao hivyo ana jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa anaongeza kipato kwaajili ya kusaidia familia yake. “Kwa muda mrefu sasa mume wangu anaishi mbali na familia, mimi ndiye niliye beba jukumu la kulea watoto wetu kwa kuhakikisha wana pata lishe bora, wana kwenda shule pia wanapata huduma za matibabu wanapokuwa wagonjwa”, alifafanua.

Aliendelea kusema kuwa, mradi wa ufugaji nyuki utasaidia kuongeza kipato na kuboresha maisha ya familia. Ni kweli serikali imetangaza elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, lakini bado kuna gharama za vifaa vya shule, pia ninapenda watoto wangu wasiishie kidato cha nne, natamani kuona watoto wangu wakipata elimu cha chuo kikuu, na haya yote yanahitahitaji fedha. Ni vyema nikaanza sasa kuwekeza kwaajili ya gharama za elimu ya juu.

Kazi ya Ufugaji nyuki hapa kijijini hufanywa na wanaume, hii ni kutokana na ugumu wa shughuli yenyewe. Lakini mafunzo yaliyotolewa na LEAT ya namna bora ya ufugaji nyuki yameondoa woga wa  wanawake walishiriki, kunamwamko mkubwa na utayari wa wanawake kujiunga na vikundi vya ufugaji nyuki. Kazi ya ufugaji nyuki imeonekana kuwa rahisi kutokana na uwepo wa mavazi ya kujikinga na nyuki pamoja na mizinga ambayo inaendelea kugawiwa bure kwa washiriki wote.


Baadhi ya mizinga ya kufugia nyuki iliyo gawiwa kwa wanavikundi vya ufugaji nyuki, kabla ya kutundikwa
 
Kuhusu nafasi ya mwanamke katika usimamizi wa maliasili, alisema amejifunza umuhimu wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda na kusimamia maliasili. Katika hilo, anaona jukumu kubwa alilonalo mwanamke katika usimamizi wa maliasili kwa kuwa mama ndiye mtumiaji mkubwa wa rasilimali hizo na zinapo haribiwa mama ndiye anapata athari kubwa.

Uharibifu wa maliasili huathiri watu wote hata viumbe hai wanao ishi kwa kutegemea uwepo wa maliasili hizi. Alimtaja mama kuwa ndiye anaye athirika zaidi kwa sababu, misitu huhifadhi vyanzo vya maji, hivyo inapo haribiwa vyanzo vya maji hukauka na mwanamke hulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji hivyo hupoteza muda mwingi pia ni hatari kiafya na kiusalama.

Kutokana na athari hizo mwanamke anapaswa awe mstari wa mbele kuhamasisha jamii kushiriki katika usimamizi wa maliasili. Kwa bahati mbaya ushiriki wa wanawake ni mdogo, hii inapunguza uzito wa athari za uharibifu wa maliasili kwa jamii. ‘Kulingana na uzoefu wangu ni kuwa madhara yeyote yanapewa uzito iwapo waathirika wataelezea athari hizo’. Mimi kama mama napaswa kuwajibika kueneza elimu ya ushiriki wa wananchi katika usimamazi wa maliasili, nahasa rasilimali misitu.

'Huwa nahamasisha wananwake wenzangu tunapo kutana katika vikao vyetu, lakini nimepewa changamoto ya kuongeza wigo wa kuhamasisha katika mikutano ya hadhara ya kijiji, ili hata wanaume waelewe ni jinsi gani uharibifu wa maliasili utaathiri wanawake'.

Mimi na wanawake wenzangu tulio pata fursa ya kushiriki mafunzo, tunalo jukumu kubwa la kuhamasisha umuhimu wa jamii kutunza maliasili zilizopo kwasababu maliasili zikiharibiwa kurejesha hali ya awali ni gharama na huchukua muda mrefu, wakati huo jamii ikiendelea kupata taabu.

'Naamini mwanamke ni mtu muhimu katika uhamasishaji wa mambo mbalimbali katika jamii, pia wanawake wakiamua kusimamia jambo mara nyingi huhakikisha kuwa jambo hilo linafanikiwa', alisisitiza.
Jumla ya vikundi 16 vya ufugaji nyuki vimepatiwa mafunzo katika wilaya mbili za Iringa vijijini na Mufindi ambako mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili utatekelezwa. Pi jumla ya mizinga 350 imegawiwa kwa wanavikundi na tayari imekwisha tundikwa. Mizinga 350 ni sawa na asilimia hamsini ya lengo la mradi ambalo ni kugawa mizinga 700, katika kipindi cha mradi.
 
 

 

 


 

No comments:

Post a Comment