Wednesday, May 11, 2016

TUNASONGA MBELE-MAFUNZO YA UFUGAJI NYUKI IFWAGI-Wilaya ya Mufindi-Iringa


 MAFUNZO YA UFUGAJI NYUKI IFWAGI-Wilaya ya Mufindi, Iringa
Kikundi cha ufugaji nyuki cha watu 22 cha kijiji cha Ifwagi, wilaya ya Mufundi chapatiwa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa siku tatu, pamoja na mizinga 22 ya kufugia, na vifaa vya kujikinga na nyuki ambavyo ni kofia, wavu wa kujikinga usoni, glavu, na viatu maalumu. Pia walipatiwa  patasi na nta.

 Baada ya mafunzo wanakikundi cha ufugaji nyuki, Afisa Nyuki wa wilaya ya Mufindi, mwakilishi wa Asasi ya ASH-TECH pamoja na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazinigira kwa vitendo(LEAT), walitembelea msitu wa asili wa Kidege ili kuainisha eneo litakalo tundikwa mizinga ya nyuki.

 Mafunzo ya ufugaji nyuki yanawapatia wakazi wa kijiji cha Ifwagi chanzo mbadala cha mapato, ilikupunguza utegemezi wa mapato yatokanayo na rasilimali za msitu wa asili wa kidege. Msitu wa asili wa Kidege unategemewa na vijiji vitatu ambavyo ni Ifwagi, Mwitikilwa na Ludilo.


Mradi wa ufugaji nyuki utasaidia kupunguza utegemezi wa mapato unaotokana na rasilimali misitu na wanyamapori katika vijiji ambavyo vinatekeleza mradi wa 'Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili', unaotekelezwa na LEAT katika vijiji 32 vya wilaya za Iringa na Mufindi, mkoani Iringa.

 
 Mradi wa Ushiriki wa Wananachi katika Usimamizi wa Maliasili unafadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID), ulianza Novemba 2014 na unatarajiwa kukamilika Novemba 2017.

Baadhi ya Wanakikundi wakiwaonesha wenzao namna ya kutundika mzinga wa nyuki baada ya mafunzo. Aliyevaa koti jeusi ni Afisa Nyuki wa Wilaya ya Mufindi bwana Hamis Hassan.
 
Wanakikundi wakifuatilia mafunzo
Wanakikundi wakiwa na Afisa Nyuki wa Wilaya ya Mufindi, Hamis Hassan (wa pili kushoto) Boksi jeupe linalo ning'inia kwenye mti ni moja ya mizinga iliyogawiwa na LEAT kwa kikundi hicho.
 
.

 

No comments:

Post a Comment