Saturday, May 7, 2016

LEAT YAGAWA VIFAA VYA UFUGAJI NYUKI


Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT) imegawa vifaa vya ufugaji nyuki katika vijiji ambayo vinatekeleza mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, unaofadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). Mradi huu unatelekezwa katika vijiji 32 vya wilaya za Iringa na Mufindi, mkoani Iringa.

Mradi wa ufugaji nyuki unalenga kusaidia jamii zilizozungukwa na rasilimali misitu na wanyamapori, kujipatia kipato mbadala ilikupunguza utegemezi wa kipato unaotokana na maliasili zilizo wazunguka.

Mradi wa ufugaji nyuki umelenga kuwafikia wananchi 700, kwa kupatiwa mafunzo ya ufugaji nyuki pamoja na kupewa mizinga na vifaa vya ufugaji nyuki. Kila mwananchi aliyepatiwa mafunzo hayo, hupewa mzinga mmoja na vifaa, ikiwemo kofia, wavu wa kuzuia kuumwa na nyuki, suti, glavu na viatu maalum.

Vifaa vya ufugaji nyuki na mizinga hugawiwa kwa awamu tofauti, kwa awamu hii jumla ya vijiji nane vimefikiwa. Vijiji hivyo ni Malinzanga, Kiwere,Mfyome, Kitapilimwa, Itagutwa, Tungamalenga, Kitisi na Idodi.

Afisa Ugani wa LEAT Hna Lupemba (kulia) akigawa vifaa vya uafugaji nyuki kwa wanakikundi wa kijiji cha Tungamalenga, wilayani Iringa

Mmoja wa wanakikundi caha ufugaji nyuki wa Tungamalenga akisaidia kumvalisha mwenyekiti wa kijiji
Mwenyekiti wa kijiji cha Tungamalenga akiwa katika mavazi ya ufugaji nyuki
Baadhi ya vifaa vya ufugaji nyuki vilivyo gawiwa kwa wanakikukndi, kijijini Tungamalenga

No comments:

Post a Comment