Monday, June 12, 2017

MAZINGIRA NI LAZIMA YAHIFADHIWE.




Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Amina Masenza kwa mara nyingine amesisitiza kuwa Mazingira katika Mkoa huo ni lazima yahifadhiwe na kulindwa kwani itasababisha baadhi ya wananchi kuathiriwa kwa namna mbalimbali endapo wataendelea kufanya shughuli zinazoathiri Mazingira.


Mkuu wa Mkoa ametoa Msimamo huo katika kilele cha wiki ya Mazingira ambayo Kimkoa imeadhimishwa katika kijiji cha Mangalali wilaya ya Iringa.


Katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala Msaidizi idara ya Mipango, Bw. Nuhu Mwasumilwe, Mkuu wa Mkoa ametoa changamoto kwa wataalam kufikiri tofauti ili kuja na njia mbadala itakayosaidia kupunguza shughuli zinazosababisha uharibifu wa Mazingira. Na hii ni kutokana na ukweli kuwa, kwa sasa kila mmoja ameshaguswa na athari zinazosababishwa na uharibifu wa Mazingira.



Afisa Maliasi wa Mkoa wa Iringa amesema baadhi ya shughuli zinazofanywa ili kusaidia uhifadhi wa Mazingira ni pamoja ufugaji wa nyuki ambapo mpaka sasa Mkoa unakadiriwa kuwa na mizinga elfu thelathini (30,000) ya watu na vikundi mbalimbali ambapo Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira (LEAT) kupitia mradi wake wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani USAID, ni moja ya wadau waliochangia mizinga hiyo kwa kutoa mizinga 704 kwa vijiji 32 Mkoani Iringa.

 Kikundi cha sanaa Mashujaa kutoka Mfyome wilayani Iringa, wakihamasisha wananchi kutunza mazingira katika kilele cha siku ya mazingira duniani, ambayo kimkoa ilihadhimishwa kijiji cha Mangalali, mkoani Iringa.

 Mgeni Rasmi, Katibu Tawala Msaidizi idara ya Mipango, Bw. Nuhu Mwasumilwe akipanda mti ikiwa kama kumbukumbu ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani katika kijiji cha Mangalali, wilayani Iringa.

 Kikundi cha sanaa Mashujaa kutoka kijiji cha Mfyome wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuamaliza tukio la kupanda mti wa kumbukumbu katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, kijiji cha Mangalali, Mkoani Iringa.

Afisa Habari na Mawasiliano kutoka LEAT akitoa salamu katika maadhimisho ya kilele cha siku ya mazingira duniani, ambayo kimkoa yalifanyika kijiji cha Malangali, wilayani Iringa, Mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment