Emmanuel Hayuka - LEAT
Japokuwa kwa wakati huu, kwa kiwango kikubwa kuna muafaka mkubwa duniani kote kuhusu uwepo wa mabadiliko ya tabia nchi katika sayari hii tunayoishi. Lakini lipo kundila watu ambalo pia ni weledi wa fani mbalimbali,
Mashaka
Lakini, ukweli wa mambo ni kwamba, “mabadiliko ya tabia nchi” ni jambo dhahiri, linaloendelea kuikabili dunia, na hasa athari zake zimekuwa zikijidhihirisha katika nchi zinazoendelea, hasa kutoka bara la
Ufahamu wa dhana ya Mabadiliko ya Tabia Nchi
Bila shaka dhana ya “mabadiliko ya tabia nchi” ni miongoni wa dhana ambazo zimekuwa vinywani kwa watu wengi duniani katika miongo ya hivi karibuni. Hii inajumuisha wale wote wanaojiusisha na masuala ya mazingira na hata wale ambao hawajihusishi nayo. Lakini wengi wetu, pengine tumekuwa tukifanya hivyo bila kujua maana, japo kwa ufupi wa dhana hii. Kuelezea kikamilifu maana ya dhana ya “mabadiliko ya tabia nchi” katika makala fupi kama hii ni jambo lisilowezekana, kwa kuwa dhana hii ni pana
Kwa mujibu wa nyaraka ya Dr.Furaha N. Lugoe wa Dar es Salaam Institute of Land Administration and Policy Studies (DILAPS) yenye kichwa cha habari “Mitazamo na Ukweli wa Mabadiliko ya Tabia Nchi”(Climate Change Perspectives and Realities), alioutoa katika warsha inayohusu “Mabadiliko ya tabia nchi” iliyoandaliwa na Citizen’s Global Platform tarehe 26 Novemba 2009, Dar es Salaam, “Mabadiliko ya tabia nchi yanachangiwa sana na ‘ongezeko la joto duniani’ (global warming). ‘Ongezeko la joto duniani’ husababishwa na kuwepo ziada ya hewa za ukaa angani ambazo zinabadilisha viwango vya nishati ya joto na hivyo kusababisha wastani wa hali ya joto angani kwa msimu kuongezeka.
‘Ongezeko la joto duniani’ni jambo linalosababishwa na mwako wa nishati kama vile; petroli, dizeli, gesi asilia, makaa ya mawe na kuni, na kadhalika; kuoza kwa mboji katika maziwa na mashamba ya mpunga na utoaji wa hewa za ukaa kutoka katika mbolea za viwandani, viwanda na vyombo vya usafiri. Hewa za ukaa vilevile hujulikana
Dr. Lugoe anafafanua zaidi kuwa, “Kwa kawaida, wakati miali ya jua inapopenya katika angahewa, sehemu mojawapo ya mnururisho wa jua unaakisiwa na kurudishwa tena angani na tabaka la juu la angahewa au ufyonzwa na tabaka la ozoni. Sehemu nyingine inapelekwa juu ya ardhi na kubadilishwa kuwa miali isiyoonekana au joto. Halafu mawingu, mvuke wa maji katika angahewa na ‘hewa za nyumba ya kijani’ zinavyonza na kuhifadhi kiwango kikubwa cha joto kinachozalishwa, hatima yake ni kuongezeka kwa joto duniani.”
Kwa upande mwingine ‘ongezeko la joto duniani’ linatokea pale chembe ndogo ndogo za chlorofluorocarbons (CFC) zinapobadilisha mtungo wa tabaka la ozoni. Kwanza, mnururisho wa miali isiyoonekana(ultra-violet radiation) inasababisha chembe ndogo ndogo za chlorofluorocarbons(CFC) kutoa chembe ndogo za chlorine(Cl) ambazo baadae zinavunja chembe ndogo za ozoni katika namna ileile ambayo miali isiyoonekana (ultra-violet radiation) ingeweza kufanya.Baadae Chroline inaungana na chembe ndogo za oxygen na kutengeneza Chlorine monoxide (ClO) ambayo inazuia utengenezwaji wa tabaka la ozoni.
Kwa hiyo, chembe huru za oxygen kwa kasi zinaunganika na Chlorine monoxide (ClO), baadae zinatoa chembe huru za Oxygen na Chlorine. Mchanganyiko huu wa kikemikali hauruhusu kutengenezwa kwa ozoni. Matokeo yake ni kwamba unene wa tabaka la ozoni unapunguzwa na hatimaye mnururisho wa miali mikali ya jua isiyoonekana (ultra-violet radiation) inaruhusiwa kufika kwenye uso wa dunia. Hali hii inachangia kuleta “ongezeko la joto duniani” ambayo pia inachangia
‘Mabadiliko ya tabia nchi’ ambayo kwa kiwango kikubwa yamesababishwa na ‘ongezeko la joto duniani’ inafanya kubadilika kwa mikondo ya mvua, kubadilika kwa kina cha bahari, kubadilika kwa mwelekeo na kasi ya upepo, kubadilika kwa mwelekeo na kasi ya mikondo ya maji ya bahari, kubadilika kwa misimu na kuongezeka kwa uwezekano wa kutokea kwa maafa ya tabia nchi kama vile; ukame, kimbunga na mafuriko.
Jambo la msingi la kuzingatia hapa ni kwamba maana hii fupi ya “mabadiliko ya tabia nchi” iliyokaririwa humu haina kusudio la kuwa maana mahsusi ya dhana hii duniani kote au miongoni mwa wanasayansi, wahandisi na wanaharakati wa mazingira. Isipokuwa kutoa mwangaza kwa umma kutambua kwa ufupi maana ya dhana yenyewe na hivyo kuwawezesha kufahamu juu ya mabadiliko ya tabia nchi na jinsi yanavyoathiri maisha yetu kwa ujumla.
Ushahidi wa mabadiliko ya tabia nchi
Ni jambo muhimu
Ushahidi wa “mabadiliko ya tabia nchi” umepatikana kutoka vyanzo mbalimbali ambavyo vinaweza kutumika kuitengeneza tena tabia nchi ya zamani ili kuweza kufanya ulinganifu. Inasemekana kuwa rekodi zilizokamilika za takwimu zinazohusu joto la uso wa duniani ulianza kuhifadhiwa katikati na mwishoni wa miaka ya 1800.
Kuna ushahidi mwingi
Ukweli wa mambo ni kuwa, uthibitisho wa “mabadiliko ya tabia nchi” ni mwingi
Uthibitisho wa baadhi ya ushahidi huo wa “mabadiliko ya tabia nchi” ni kutokea kwa mafuriko makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa kwa kipindi kirefu katika sehemu mbalimbali duniani. Mafuriko ya Mto Rhine (Ulaya magharibi) kati ya mwaka 1996 na 1997, mafuriko ya China ya mwaka 1998, mafuriko ya Ulaya mashariki ya mwaka 1998 na 2002, mafuriko ya Msumbiji na Ulaya ya mwaka 2000 na mafuriko ya Bangladesh yaliyosababishwa na mvua za mansuni mwaka 2004 ambayo yalifanya takribani asilimia sitini (60%) ya nchi kuwa chini ya maji na hata mafuliko makubwa yaliyoikumba Ufilipino mwaka huu (2009) ni mojawapo ya mifano inayothibitisha uwepo wa dhana ya “mabadiliko ya tabia nchi”.
Mathalani, utafiti wa kisayansi unaonyesha bayana kuwa kiwango cha ujazo wa maji katika maziwa makubwa ya Afrika kama vile Ziwa
Mbali ya hayo, kuna uthibitisho mwingine unaodhihirisha kuwepo kwa “mabadiliko ya tabia nchi” duniani na hata Afrika ni kuongezeka kwa kasi ya kuyeyuka barafu. Utafiti wa kisayansi unaonyesha barafu imeyeyuka kwa kiwango kikubwa
Jambo kama hili pia linatokea nchini
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro na Bwana Lonnie Thomson, mtaalamu wa Sayansi ya Theluji (Glaciologist) anayefanya kazi zake katika kituo kiitwacho Byrd Polar Research Centre, Columbus (Kituo cha Utafiti wa Theluji cha Byrd) kilichopo katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Ohio (Ohio State University) unaonyesha kwamba kuyeyuka kwa theluji ya Mlima Kilimanjaro unaendelea kwa kasi kubwa.
Utafiti huo umebaini kuwa zaidi ya robo ya kiwango cha theluji kilichoufunika Mlima Kilimanjaro mwaka 2000 kilipotea ilipofika mwisho wa mwaka 2007. Bwana Thompson na washirika wake walitoa ripoti hiyo tarehe 2 Novemba 2009, katika mhadhara uliondaliwa na Chuo cha Kitaifa cha Sayansi cha Marekani (National Academy of Science).
Takwimu zilizopatikana kutokana na utafiti uliofanywa angani umeongezea takwimu zilizokusanywa na timu ya utafiti ya Bwana Thompson na washirika wake. Takwimu hizo zinaonyesha kwamba uyeyukaji wa theluji katika Mlima Kilimanjaro uliongezeka kwa kiasi kikubwa miongo ya hivi karibuni, anasema Bwana Thompson. Inasemekana kuwa kuanzia mwaka 1912 hadi 1953 theluji inayofunika Mlima Kilimanjaro ilipungua kwa kiwango cha 1.1% kwa mwaka. Vivyo hivyo, kati ya mwaka 1953 na 1989 wastani wa kiwango cha kupungua kwa theluji kwa mwaka kiliongezeka na kufikia 1.4%.
Tokea utafiti ulifanywa mwaka 1989 hadi kufikia utafiti uliofanywa hivi karibuni, mnamo mwaka 2007 umeonyesha kupungua kwa kiwango kikubwa cha eneo la Mlima Kilimanjaro lililofunikwa na theluji, kwa wastani mkubwa sana cha 2.4%, wanabainisha watafiti hao.
Bwana Thompson anasema, siyo tu kwamba mapande makubwa ya theluji kwenye kilele cha mlima yamekuwa yakipungua, yanapungua kwa kasi kubwa, mwelekeo huu umegundulika tu kwa kutumia njia ya utazamaji kutokea ardhini iliyoboreshwa miaka ya hivi karibuni.
Sehemu pana zaidi ya kilele ambayo inakadiriwa kuwa na upana wa meta 50 iitwayo “Ukanda wa Theluji wa Kaskazini”, imekuwa ikipungua kwa kiwango cha meta 1.9 kati ya mwaka 2000 na 2007. Kwa kipindi hicho hicho, “Ukanda wa Theluji wa Kusini” wa mlima Kilimanjaro ambao unakadiriwa kuwa na upana wa meta 21 mwaka 2000, umepoteza meta 5.1 ya unene wa theluji mwaka 2007.
Bwana Thompson anaongeza kuwa,
Hata Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Jamhuri ya Muungano wa
Kutokana na uthibitisho huu, sidhani kama kuna mtu yoyote atakayeshindwa kung’amua nini itakuwa hatima yake kwa dunia, na hasa
Nini kisababishacho
Kuna nadharia kadha wa kadha zinazojaribu kuelezea sababu zinazosababisha mabadiliko makubwa ya tabia nchi yanayoendelea kushuhudiwa sasa ulimwenguni kote. Miongoni wa sababu zinazotajwa kuwa ndizo zimepelekea kuwepo kwa “mabadiliko ya tabia nchi” ni; mabadiliko ya mnururisho wa jua, mchepuko wa sayari ya dunia katika mzunguko wake, mtengenezeko wa milima na mwelekeo wa mabara, kubadilika kwa mkusanyiko wa pamoja wa gesi inayoathiri hali ya hewa kutokana na shughuli za binadamu.
Kitaaluma sababu zote hizo na nyingine ambazo hazija orodheshwa humu ni muhimu
Kwa sasa kuna muafaka wa kisayansi kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi, kwamba shughuli za binadamu inawezekana zikawa ni sababu kubwa ya kuongezeka kwa kasi kubwa
Vivyo hivyo, mchakato huo wa kuongezeka kwa hewa ya ukaa (carbon dioxide) na gesijoto angani unachangia uharibifu wa “tabaka la ozoni” (ozone layer) ambalo limekuwa likiikinga dunia na kunururishiwa miale mikali ya jua. Jambo hili pia husababisha ongezeko la joto duniani na hatimaye “mabadiliko ya tabia nchi”.
Sababu nyingine ya “mabadiliko ya tabia nchi” ni ukataji mkubwa usio endelevu wa misitu (deforestation). Hali hii pia inachangia
Shughuli za binadamu zinazochangia ongezeko la joto duniani na hatimaye “mabadiliko ya tabia nchi” ni nyingi mno, mbali na hizi zilizotajwa, zingine ni
Namna za kutatua
Ni ukweli usiopingika kwamba ulimwengu unakabiliwa na mabadiliko makubwa ya tabia nchi. Kama tulivyoona hapo juu, mbali na sababu za kiasili, vilevile shughuli za binadamu zimekuwa ni sababu kubwa
Kutokana na ukweli huu hata utatuzi wa jambo hili pia unategemea namna ya kuikabili sababu hii kubwa inayochangia kuwepo kwake. Ndiyo maana, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Ni dhahiri kwamba kauli hii ya Rais Kikwete imelenga kwenye kitovu cha chanzo cha tatizo la “mabadiliko ya tabia nchi”. Kwa hali hii ni jambo la msingi kujua namna ambavyo gesijoto hasa hewa ukaa ambazo husababisha ongezeko la joto dunia na hatimaye “mabadiliko ya tabia nchi”, zinavyoweza kupunguzwa.
Bwana Emmanuel Massawe, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira (Lawyers’ Environmental Action Team, LEAT) ametoa kauli inayoshahabiana kwa kiwango kikubwa na ile ya Mheshimiwa Rais Kikwete, kwamba, “Mabadiliko ya tabia nchi yanayoshuhudiwa duniani kwa sasa, inawezekana kuepukwa kwa kuhakikisha kwamba ongezeko la joto duniani linapunguzwa na kudhibitiwa. Jambo hili linawezekana tu, kwa kupunguzwa kiwango cha utoaji wa hewa ukaa na gesijoto angani ambazo zinachangia
Bwana Massawe, anaongeza kuwa jambo ili litawezekana
“Nadhani utekelezaji wa Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji miti hovyo na uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) utasaidia
Mpango huu (MKUHUMI) unatokana na Jumuia ya Kimataifa kutambua kwamba, kama misitu itajumuishwa katika utatuzi wa “mabadiliko ya tabia nchi”, hivyo nchi zinazoendelea lazima zifidiwe kwa kuhifadhi na kupunguza ukataji wa misitu unaotokea pale misitu inavyokatwa kwa matumizi mengine ya ardhi hiyo, pamoja na uharibifu wa misitu unaotokea pale maliasili za misitu zinavyoharibiwa. Kwa kuwa, ardhi yenye misitu inaweza kuwa na thamani kutokana na uuzaji wa mbao uletao fedha za kigeni kwa taifa au uwezekano wa kutumika kwa kilimo cha mazao ya biashara na chakula kwa ajili ya kulisha idadi ya watu inayoongezeka kila siku. Hivyo ni muhimu kutoa tuzo ya fedha ili kuhakikisha kuwepo misitu hiyo kwa kuwapa wananchi hamasa ya kuihifadhi, kuitunza na kuitumia kiuendelevu.
Mchango wa misitu katika kutatua tatizo la “mabadiliko ya tabia nchi” ni kutokana na ukweli kwamba misitu hufyonza hewa ukaa na hivyo kupunguza mlundikano wake angani. Inakadiriwa kuwa asilimia ishirini (20%) ya utoaji wa hewa ukaa angani unaweza kupunguzwa kwa kutokata na kuharibu misitu. Vilevile misitu inaweza kuchangia katika kukabiliana na “mabadiliko ya tabia nchi” kwa kuipatia dunia huduma ya ikolojia.
Hivyo, Bwana Massawe anafafanua zaidi kuwa, “Sisi LEAT tunauona MKUHUMI kuwa wenye manufaa
No comments:
Post a Comment