Monday, January 25, 2016

LEAT YAWAJENGEA UWEZO WADAU WA UTEKELEZAJI WA MRADI WA USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA KUSIMAMIA MALIASILI

Timu ya wanasheria watetezi wa mazingira LEAT imewajengea uwezo mashirika ya kijamii katika kuandaa mipango kazi pamoja na bajeti, katika wilaya za Iringa vijijini na Mufindi, mkoani Iringa.

Mafunzo hayo ni njia moja wapo ya kurahisisha utekelezaji wa mradi wa Ushiriki wa wananchi katika Usimamizi wa Maliasili. Mradi huo umefadhiliwa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia shirika la maendeleo la watu wa marekani(USAID). Huu ni mradi wa miaka minne, ulianza kutekelezwa mwaka 2014 unatarajiwa kukamilika mwaka 2017.

Lengo la mradi huu ni kuwajengea uwezo wananchi iliwaweze kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa maliasili (misitu na wanyama pori) kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya.

Mpaka sasa LEAT imewajengea uwezo takriban wadau 1500, ikiwa ni pamoja na wananchi wa kawaida, viongozi wa vijiji, kakamati za ardhi, kamati za maliasili za vijiji na wilaya.

Wadau wa utekelezaji wa mradi walio jengewa uwezo ni kutoka Iringa vijijini ni taasisi za MBOMIPA na MJUMIKK na Mufindi walikuwa ASH-TECH na MUVIMA.
 
Thomas Mtelega, Afisa Programu wa ASH-TECH akiwasilisha mapango kazi wa taasisi yao
Afisa Mradi wa LEAT, Musa Msanizu (katikati) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa ASH-TECH Erasto Mazela (kulia) na Afisa Programu wa ASH-TECH, Thomas Mtelega
Afisa Mradi Mwandamizi wa LEAT, Remmy Lema akimwelekeza Afisa Mradi wa MUVIMA, Winnie Moses namna ya kutengeneza bajeti ya mradi
 

Wednesday, May 6, 2015

LEAT KUTUMIA VIKUNDI VYA SANAA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KATIKA USIMAMIZI WA MALIASILI

Sanaa kwa maendeleo ni dhana ya kutumia sanaa hasa  za  maonesho ili kumuwezesha mwanajamii kujiletea maendeleo yake mwenyewe.
Mbinu ya sanaa kwa maendeleo imejikita zaidi katika kuamini kuwa ikiwa jamii Fulani ina matatizo ya kimaendeleo, ni wanajamii wenyewe ndio wana uwezo wa kuyajadili na kuyatafutia ufumbuzi matatizo hayo. Ingawa dhana hii sio ngeni sana masikioni mwa wnajamii na wanaharakati mbalimbali wa maendeleo imekuwa ikitumika kama kielelezo kuonesha mchango wa sanaa katika kuleta maendeleo ya mtanzania.
LEAT inaamini kuwa sanaa ni chombo kinachoweza kuionesha jamii jinsi ilivyo kwani sanaa kwa maendeleo ni zao la jamii lenyewe. Kwa kuliona hili LEAT kupitia nradi wa ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa maliasili imetoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya sanaa katika wilaya za Iringa Vijijini na Mufindi. Lengo la mafunzo haya ni kuvijengea uwezo vikundi hivi kutumia fani mbalimbali za sanaa zilizopo katika jamii husika kama vile ngoma, hadithi, maigizo,nyimbo mashairi, viziga na nyinginezo  katika kuamsha ari na kuwawezesha wanajamii kupata fursa ya kujadili na kuhoji mambo mbalimbali hasa yanayohusu usimamizi wa maliasili ambayo yamekuwa kikwazo cha maendeleo.
Sanaa shirikishi inalenga kuhakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu katika shughuli za kujiletea maendeleo . Kama sanaa ikitumika vizuri inaweza kuwahamasisha wanajamii kuinuka  na kuweza kuwawajibisha viongozi wazembe pale wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao.
Mafunzo haya  kwa vikundi vya sanaa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Ushiriki wa  Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili(CEGO-NRM)  wenye lengo ka kuwawezesha wananchi kushiriki katika usimamizi wa maliasili na kuweza kuwajibisha viongozi na mamlaka mbalimbali zenye dhamana ya kusimamia maliasili pale zinaposhindwa kutekeleza majukumu yake. Mafunzo haya yalifanyika katika kata mbili, Kata ya Kiwere iliyopo wilaya ya Iringa Vijijini na kata ya Igombavanu iliyopo wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, Mafunzo yalianza katika Kata ya Kiwere tarehe 24- 27 Aprili 2015 na Kisha kwenda katika Kata ya Igombavanu tarehe 29 Aprili-1Mei 2015. Baada ya Mafunzo haya LEAT inategemea kuvitumia vikundi hivi vya sanaa katika kufanya maonesho yanayohusu ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa maliasili na ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii.
Mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili unafadhiliwa na USAID na  unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mi nne (4) katika wilaya za Iringa Vijijini na Mufindi mkoani Iringa.

Thursday, October 9, 2014


LEAT received 95.9 Million Tshs from Legal Services Facility (LSF) as grants to implement a project on Advocacy for reducting economic gender based violence. This is a twelve (12) Months project started from September 2014 to August 2015, implemented in Dodoma Region at Mpwapwa specifically in six (6) villages in three Wards including Kibakwe, Ipera and Rudi. The project target groups are women and men aged 15years and above and the project is intended to benefit 150 beneficiaries in the entire districts which is 25 citizens each villages.
The main objective of the project is to create the community with fair distribution, ownership and control of economic resources. Specifically the project aimed at increasing the community awareness on Economic Gender Based Violence (EGBV) at domestic level and legal rights access to resources as well as linking women and girls with legal institutions to protect them, and respond to Economic Gender Based Violence (EGBV)
LEAT will work to create a better environment for upholding, respecting, and defending the rights of the rural women and girls in Mpwapwa district and enable them to know, advocate and defend their human rights including life to life, right to decent treatment and respect, equality before the law, right to own property, freedom association and expression right to take part in decision making process at the family, village, district and national level, Duty to enforce the law, right to privacy, freedom of movement, right to work and livelihood, right to have a family and many among others”. Said Glory Baltazari Kilawe (Advocate) who is also the coordinator for this project.
During the implementation of this project LEAT will conduct weekly sessions to peer group on EGBV and legal rights, organizing and conducting trainings of facilitators (TOF)/Peer educators on EGBV and legal rights. Conducting public sensitization meetings through theater for development, produce training manuals on EGBV as well as monitoring and evaluation of the project activities.
LEAT intervention will result to the empowerment in the aspects of Economic Gender Based Violence, Human rights and legal right in the project area. It will also lead to increase awareness on Economic Gender Based Violence, human rights and Legal Rights to communities in Mpwapwa District particularly in the targeted project villages. The project will lead to the identification and utilization of legal services in project villages necessary in combating Economic Gender Based Violence and enforcing of human right and legal rights. Not only that but also women and community members will vigorously report and take action against Economic Gender Based Violence (EGBV)and actively take part in decision making processes pertaining to the control distribution and ownership of resources in their respective villages and there will be reduced cases of Economic Gender Based Violence in project villages.

Tuesday, October 7, 2014

RIPOTI YA PROGRAMU YA WAKALA WA MABADILIKO


Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira (LEAT) inafanya programu ya kuiwezesha jamii kutunza Mazingira na kuibua miradi kupitia Mbinu Shirikishi ya Kujifunza kwa Vitendo (Participatory Learning and Action/People Owned Process) ambayo inasimamiwa na Asasi iitwayo Mtandao wa mazingira Tanzania  (Mazingira Network Tanzania (MANET) iliyopo Morogoro na kufadhiliwa na  Mfuko wa dunia wa wanyamapori (WWF-Norway.) MANET inafanya programu hii kwa kushirikisha Asasi mbalimbali Tanzania kwa lengo la kuwezesha jamii zote kuibua na kumiliki miradi yao wenyewe pasipo kutegemea wawekezaji au Wafadhili). MANET iliweza kuteua wakala wa mabadiliko (Young Environmentalist Trainee (YET)) kutoka kila asasi nchini Tanzania. Kutoka LEAT Bi Edina Tibaijuka ambaye ni Afisa Mazingira  na mkuu wa Idara ya  udhubiti wa taka na uchafuzi wa Mazingira. aliteuliwa kuwa  wakala wa mabadiliko(YET) na kuiwakilisha asasi kwenda kupata mafunzo hayo ya PLA/POP.

Katika harakati za kuendeleza mradi huu LEAT iliamua kutoa mafunzo haya katika kitongoji cha Majani Mapana wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani kwasababu ni moja ya wilaya inayokumbana na changamoto ya uchafuzi wa Mazingira uliosababishwa na uwepo wa dampo katikati ya makazi ya wanajamii hao. Hivyo hali hii inazidi kurudisha nyuma hali ya utunzaji Mazingira na hali ya uchumi kwa jamii ya watu wa Majani Mapana.

Hivyo tangu mwezi Oktoba 2013 hadi hivi sasa LEAT imekuwa ikishirikiana kwa ukaribu na wanajamii wa Majani Mapana katika kutoa mafunzo ya elimu shirikishi ya kujifunza kwa vitendo (PLA/POP) ili kuhakikisha wanajamii wanaweza kutatua changamoto mbalimbali za Mazingira na kuweza kubadilisha mitazamo yao juu ya utegemezi. LEAT inaamini ifikapo mwisho wa mwaka huu ambapo ndio utakuwa mwisho wa programu hii Jamii hii itaweza kujisimamia yenyewe katika kulinda Mazingira na kuendeleza miradi mbalimbali ya utunzaji Mazingira.

Monday, September 29, 2014

NOTIFICATION FOR OFFICIAL EMAIL CHANGE

Dear Followers, LEAT wishes to inform you that we have changed our official email from info@leattz.org to info@ leat.or.tz. This is due to change in website domain which is currently www.leat .or.tz. We are sorry for any inconveniences caused due to this act.
Keep in touch

Thursday, September 25, 2014

KAMATI ZA VIJIJI ZA MAZINGIRA ZAFUNZWA JUU YA USIMAMIZI WA MALIASILI KUPITIA UFUATILIAJI UWAJIBIKAJI JAMII.

KAMATI ZA VIJIJI ZA MAZINGIRA ZAFUNZWA JUU YA USIMAMIZI WA MALIASILI KUPITIA UFUATILIAJI UWAJIBIKAJI JAMII.


Timu ya wanasheria watetezi wa mazingira (LEAT) kupitia mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili ( CEGO-NRM) ambao upo chini ya Ufadhili wa Shirika la maendeleo la misaada la watu wa Marekani (USAID) inaendesha mafunzo ya Usimamizi wa Maliasili kwa kupitia dhana ya mfumo wa Ufuatiliaji wa Uwajibikaji jamii

 (UJJ/SAM) katika mkoa wa Iringa, wilaya mbili za Iringa vijijini na Mafinga.

Mafunzo yalianza mnamo mwezi wa nane na yataendelea hadi mwezi wa kumi mwaka 2014. Walengwa wakuu wa mafunzo haya ni Kamati za Mazingira za vijiji kama vile kamati za maliasili, kamati za maji, kamati za matumizi bora ya ardhi, kamati za mipango na fedha, baraza la ardhi na kamati nyingine zinazohusika na mazingira vijijini.

 Hadi sasa LEAT imeweza kuzifikia kamati hizi na kuwapatia mafunzo ambapo mpaka sasa Katika wilaya ya Iringa vijijini LEAT imeweza kuifikia kata ya KIwere na Idodi ambapo  katika kata ya Kiwere wkamati za mazingira za vijiji vya kiwere, Mfyome,Kitapilimwa na itagutwa vimenufaika na mafunzo haya, vilevile katika kata ya Idodi kamati za vijiji za Tungamalenga, idodi zimefikiwa na kuelimishwa wakati kijiji cha Kitisi kikitegemea kufikiwa na Mafunzo haya mwanzoni mwa mwezi wa kumi.

Kadhalika katika wilaya ya Mafinga LEAT imekusudia kuzifikia kata Mbili ambazo ni Igombavanu na Saadani ambapo mpaka sasa LEAT imeweza kuvifikia vijiji vya Igombavanu, uhambila Lugoda lutali na Tambalang’ombe katika kata ya igombavanu wakati katika kata ya Saadani LEAT imeweza kuvifikia vijiji vya Kibada,Mapogolo wakati kijiji cha utosi kikitegemea kufikiwa mwanzoni mwa mwezi wa kumi.

Mafunzo haya yamelenga kuwafikia angalau wajumbe 35 wa kamati za Mazingira kwa kila kijiji na lengo kuu la mafunzo haya ni

 I. Ni kuijengea uwezo jamii kufahamu mwelekeo sahihi wa uwajibikaji jamii.

 II. Kuelewa dhana ya mfumo wa uwajibikaji jamii katika usimamizi wa misitu na wanyamapori.

  III. Pia kuelewa hatua tano za mchakato wa mfumo wa uwajibikaji jamii ikwa ni pamoja na mpango wa mgawanyo wa rasilimali, usimamizi wa matumizi, usimamizi wa uadilifu na usimamizi wa uangalizi.

 Vilevile mafunzo ya ufuatiliaji na usimamizi wa uwajibikaji wa jamii yanalenga kuongeza uelewa juu ya zana za uwajibikaji na usimamizi wa jamii kwa kufuatilia kila hatua ya mchakato.

 Hivyo basi ufualiaji wa uwajibikaji jamii unawezesha watoa huduma kwa jamii kutoa ufafanuzi, uthibitisho na uhalalisho juu ya mgawanyo wa raslimali za umma, utekelezaji wake na ufanisi/utendaji wake. Lengo ni kuhakikisha kuwa viongozi wa serikali pamoja na watoa huduma wote wanawajibika na wanawajibishwa ipasavyo pale wanaposhindwa kufikisha huduma muhimu kwa jamii kama walivyoorodhesha katika mpango mkakati, Mpango mwaka na bajeti ya Mwaka ili kuweza kufikia haki za msingi za binadamu/mwananchi.

 

                       TEN JOURNALISTS TRAINED ON EXTRACTIVE INDUSTRIES

 Under TMF- lEAT extractive industries fellowship for journalists program 2014 10 fellows were trained on extractive industries

This fellowship program funded by Tanzania media fund aimed at increasing the capacity of 10 fellows on the extractive industry by equipping them with critical knowledge on mining industry and oil and gas exploration and production structure enabling them to deliver quality print articles and stimulate debates or reactions from the public and policy makers based on the published articles. this was a six months fellowship aimed at building capacity of 10 Journalists fellows on extractive industry during the six months of the fellowship, enabling them to generate quality print articles on extractive industry during the five weeks of fieldwork and 7 seven weeks after fieldwork as well as engendering change in the society through increased public awareness in well-informed debates between members of the public and policy makers during the fellowship program and soon thereafter.

The training was typically based on, the political economy of the extractive industries; the policy and legal regimes of extractive industries in Tanzania; institutions governing the extractive industries in Tanzania;

bilateral investments treaties and international investment dispute settlement mechanisms; the tax regime on the extractive industries in Tanzania; fiscal tools in international petroleum agreements (IPA), oil and gas exploration and production, natural resources governance reporting tools for journalists; environmental management policy and legal frameworks for extractive industries as well as cosmetics reforms in the mining industry in sub-Saharan African countries.

LEAT together with the donor TMF believes that Journalists trained under this fellowship program will accentuate on knowledge sharing to other journalists that have not benefited from this program and they will use the knowledge to deliver quality print articles and stimulate debates or reactions from the public and policy makers based on the published articles for the benefit of the Tanzania Community.