Tuesday, October 7, 2014

RIPOTI YA PROGRAMU YA WAKALA WA MABADILIKO


Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira (LEAT) inafanya programu ya kuiwezesha jamii kutunza Mazingira na kuibua miradi kupitia Mbinu Shirikishi ya Kujifunza kwa Vitendo (Participatory Learning and Action/People Owned Process) ambayo inasimamiwa na Asasi iitwayo Mtandao wa mazingira Tanzania  (Mazingira Network Tanzania (MANET) iliyopo Morogoro na kufadhiliwa na  Mfuko wa dunia wa wanyamapori (WWF-Norway.) MANET inafanya programu hii kwa kushirikisha Asasi mbalimbali Tanzania kwa lengo la kuwezesha jamii zote kuibua na kumiliki miradi yao wenyewe pasipo kutegemea wawekezaji au Wafadhili). MANET iliweza kuteua wakala wa mabadiliko (Young Environmentalist Trainee (YET)) kutoka kila asasi nchini Tanzania. Kutoka LEAT Bi Edina Tibaijuka ambaye ni Afisa Mazingira  na mkuu wa Idara ya  udhubiti wa taka na uchafuzi wa Mazingira. aliteuliwa kuwa  wakala wa mabadiliko(YET) na kuiwakilisha asasi kwenda kupata mafunzo hayo ya PLA/POP.

Katika harakati za kuendeleza mradi huu LEAT iliamua kutoa mafunzo haya katika kitongoji cha Majani Mapana wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani kwasababu ni moja ya wilaya inayokumbana na changamoto ya uchafuzi wa Mazingira uliosababishwa na uwepo wa dampo katikati ya makazi ya wanajamii hao. Hivyo hali hii inazidi kurudisha nyuma hali ya utunzaji Mazingira na hali ya uchumi kwa jamii ya watu wa Majani Mapana.

Hivyo tangu mwezi Oktoba 2013 hadi hivi sasa LEAT imekuwa ikishirikiana kwa ukaribu na wanajamii wa Majani Mapana katika kutoa mafunzo ya elimu shirikishi ya kujifunza kwa vitendo (PLA/POP) ili kuhakikisha wanajamii wanaweza kutatua changamoto mbalimbali za Mazingira na kuweza kubadilisha mitazamo yao juu ya utegemezi. LEAT inaamini ifikapo mwisho wa mwaka huu ambapo ndio utakuwa mwisho wa programu hii Jamii hii itaweza kujisimamia yenyewe katika kulinda Mazingira na kuendeleza miradi mbalimbali ya utunzaji Mazingira.

No comments:

Post a Comment