Tuesday, April 11, 2017

Timu ya SAM ya Wilaya ya Iringa yatoa mrejesho na tathimini ya usimamizi wa maliasili kwa Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa





Mkuu wa wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesela ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa, kutoa maelezo ama kumwajibisha Mtumishi anayekwamisha shughuli za uhifadhi wa Mazingira katika wilaya hiyo.


Kutokana ripoti iliyowasilishwa mwaka jana na Timu ya SAM ya wilaya ya Iringa inayowezeshwa na LEAT kupitia msaada wa watu wa Marekani USAID, iliweza kuibua changamoto mbalimbali za usimamizi wa maliasili na kutoa mapendekezo kwa halmashauri ya wilaya ya Iringa kujaribu kutatua changamoto hizo za kimazingira. Bw. Kasesela alisema walikubaliana mambo mbalimbali yatatekelezwa lakini mpaka hivi, asilimia 80 ya mambo hayo hayajatekelezwa kutokana na baadhi ya watumishi
kutotimiza wajibu wao.


Mkutano huo wa mrejesho wa shughuli za usimamizi wa maliasili uliofanya na Timu ya SAM ya wilaya ya Iriniga kwa kushirikiana na LEAT, ulihudhuriwa na wataalamu na Maafisa wa wilaya ya Iringa, Mkurugenzi wa wilaya na wafanyakazi kutoka LEAT. 

Afisa Mwandamizi wa mradi wa CEGO Bw. Remmy Lema alisema, Pamoja na elimu na kuwasaidia kuboresha sheria za vijiji, katika mradi wa ushiriki wa Wananchi katika usimamizi wa maliasili zao (CEGO), unaofadhiliwa na Shirika la misaada la Marekani USAID, Timu ya watetezi wa Mazingira kwa vitendo LEAT pia imetoa mizinga ya nyuki kwa vijiji kama njia mbadala ya wananchi hao kujikimu kimaisha na tayari
wameshatoa mizinga ya nyuki 704.

No comments:

Post a Comment