Wednesday, March 1, 2017

KUBADILISHANA UZOEFU- TIMU YA LEAT YAFANYA ZIARA SERENGETI

  
Timu ya LEAT wakiwa katika ofisi ya SEDEREC katika ziara ya mafunzo

Kutoka kushoto ni Afisa Ughani wilaya ya Iringa Bi. Hana Lupembe, Afisa Mradi wilaya ya Iringa Bw. Musa Mnasizu, Afisa Mradi wilaya ya Mufindi Bw. Jamal Juma, Afisa Ughani wa wilaya ya Mufindi Bw. Franklin Masika wakiwa na mwenyeji wao katika ofisi ya SEDEREC kwa lengo kujifunza katika ziara yao Serengeti




Timu ya LEAT wakiwa katika ziara ya mafunzo ofisi za Jumuiya ya Hifadhi ya wanyama pori IKONA (Ikona WMA)
Timu ya LEAT wakiwa katika mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyapori Ikona (Ikona WMA)



  Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) walishiriki ziara ili kujifunza zaidi namna ambavyo Kituo cha Tafiti za Maendeleo na Uhifadhi Mazingira cha Serengeti (SEDEREC) kinavyotekeleza dhana ya uawajibikaji kupitia mfumo wa Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii. Warsha hiyo ilifanyika tarehe 15 hadi 22 Januari 2016, katika wilaya ya Serengeti, mkoani Mara.

  Ziara hiyo ilitokana na ushauri uliotolewa na aliyekuwa Afisa Mwakilishi wa Makubaliano wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID), Mikala Laurdisen, kuwa timu ya watekelezaji wa mardi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili iende kujifunza zaidi namna timu za Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii, zinavyoweza kuwa na jukumu fanisi katika kuimarisha timu ndogo za Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii za wananchi, katika kudai uwazi na uwajibikaji kutoka kwa viongozi wao wanapokuwa wanatekeleza majukuma yao juu ya mapato yanayotokana na maliasili. Ziara ya mafunzo ilihudhuriwa na Maafisa mradi Jamal Juma na Musa Mnasizu, pamoja na Maafisa Ugani Hanna Lupembe na Franklin Masika.

  Afisa Mradi, Jamal Juma alisema kuwa timu ya LEAT ilikwenda Serengeti kujifunza katika shirika la SEREDEC. Aliongezea kuwa licha ya kuwa shirika la SEREDEC linatekeleza Mfumo wa Ufuatiliaji wa Matumizi ya Umma badala ya mfumo wa Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii, ambao ndio ilikuwa lengo la ziara ya mafunzo, timu ya LEAT ilijifunza baadhi ya masuala ambayo itayafanyia kazi.

  Timu ya LEAT ilijifunza kuwa matumizi ya miundo iliyopo ya serikali ya kijiji katika usimamizi wa rasilimali za umma ni endelevu zaidi na una gharama nafuu ikilinganishwa na uanzishwaji wa chombo kipya katika ngazi ya kijiji ambacho wakati mwingine kinaweza kikakosa msaada kutoka serikali ya kijiji wakati  wa utekelezaji wa shughuli zake.

 Timu pia ilijifunza kwamba uundaji wa kamati za Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii katika ngazi ya kijiji ufanyike kupitia makutano mkuu wa kijiji ambapo wanakijiji wote wanapaswa kushiriki kuchagua watu ambao wataunda kamati hiyo.


  Kwa upande wake Afisa Ugani, Frankly Masika,     alisema kuwa walipata changamoto ya kufikia lengo la ziara yao kwakuwa SEDEREC hawafahamu na wala hawatekelezi mfumo wa Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii, na kwakuwa SEDEREC imeelekeza nguvu zake katika kutetea migororo kati ya binadamu na wanyamapori na ufuatiliaji wa matumizi ya umma.


   Franklyn alifafanua kuwa licha ya kuwa kuna baadhi ya mambo walijifunza na kuwa yatasaidia katika utekelezaji wa mradi, alisema lengo kuu la kujifunza namna bora za utekelezaji wa shughuli za timu ndogo za Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii, halikufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

  Alisema kuwa, Timu ya LEAT na SEDEREC waliweza kubadilishana uzoefu na kuangalia ni mambo gani kila upande ynaweza kuboresha katika utekelezaji wa miriadi yao. Ambapo alisema, Timu ya LEAT iliishauri SEDEREC kuwa ili kamati za Ufuatiliaji Matumizi ya Umma ziweze kufanya kazi kwa ufanisi zinapaswa ziundwe na wanakijiji pekee ambao ndio watakao tathmini utendaji wa Maafisa wa serikali na sio kuundwa pamoja na Maofisa wa serikali. Hiyo itaongeza ufanisi katika ufuatiliaji kwakuwa ni vigumu sana mtu kujifanyia tathmini ya utendaji wake.




No comments:

Post a Comment