Tarehe 25 April 2016 Timu ya Wanasheria Watetezi wa
Mazingira kwa vitendo (LEAT) kwa kushirikiana na wananchi wanaoishi katika
vijiji vinavyotekeleza mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa
Maliasili, waliendesha kipindi cha kwanza cha mradi. Kipindi hicho kilirushwa
kupitia redio Nuru FM 93.5 ya mjini Iringa.
Wadau wa mradi katika studio za redio Nuru FM, kutoka kushoto: Afisa Mradi, Musa Mnasizu, Chuki Mduda na Hamza Chang'a.
Katika kipindi hicho Afisa Mradi wa LEAT, Musa Mnasizu
alianza kwa kuelezea historia fupi ya taasisi ya LEAT pamoja na shughuli zake.
Musa pia alieleza lengo la mradi, mafanikio na changamoto katika usimamizi wa
maliasili.
Kwakuwa mradi unatekelezwa na wadau mbalimbali wakiwemo
wananchi, wakazi wawili wa Wilaya ya Iringa bwana Chuki Mduda kutoka kijiji cha
Mfyome, pamoja na bwana Hamza Chang’a kutoka kijiji cha Kiwere walishiriki
katika kipindi hicho.
Vipindi vijavyo vitafanyika kama ifuatavyo. Jumanne tarehe 9 Mei na kurudiwa Ijumaa tarehe 13 Mei 2016. Baada ya hapo kipindi kingine kitakuwa tarehe 16 Mei na kurudiwa tarehe 20 Mei 2016. Tafadhali usikose kusikiliza vipindi hivi. Utapata fursa ya kuuliza maswali au kuchangia mjadala.
Pia unakaribishwa kutoa maoni kuhusiana na kipindi hiki.
Usokitabu: facebook/leat.com
No comments:
Post a Comment