Tarehe 8 Mei 2016, Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) iligawa mizinga 22 kwa kikundi cha wafugaji nyuki 22 wa kijiji cha Ludilo, wilayani Mufindi katika mkoa wa Iringa.
Wanakikundi pia walipatiwa nyenzo muhimu iliwaweze kutekeleza kazi hiyo kwa ufanisi. Nyenzo hizo ni pamoja na suti maalum, kofia, wavu wa kujikinga usoni, glavu, viatu, patasi na nta.
Kabla ya kugawiwa mizinga kikundi kilipatiwa mafunzo ya siku tatu ya ufugaji nyuki ambapo walijifunza namna bora ya ufugaji nyuki, aina za nyuki na umuhimu wa asali kwa matumizi ya kila siku. Pia, kikundi kitapatiwa mafunzo ya namna ya kufungasha asali na utafutaji masoko.
Kutokana na umihumu wa asali kwa matumizi ya kila siku, kumekuwa na mwamko mkubwa wa watu kutumia asali, hali hiyo inatoa fursa za ajira kwa wakazi wa maeneo yanayofuga nyuki.
Mradi wa ufugaji nyuki ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, unaotekelezwa na Timu wa Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).
Moja ya lengo la mradi ni kuhakikisha kuwa Wananchi wanaoishi katika maeneo yenye rasilimali misitu na wanyamapori wanashiriki kikamilifu kuhifadhi na kulinda maliasili hizo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Ilikufikia lengo hilo, mradi wa ufugaji nyuki ni moja ya njia zitakazo wasaidia wananchi kupata vipato bila ya kutegemea rasilimali misitu, na wanyamapori; ilikuwa na mpango dumivu wa rasilimali hizo.
Afisa akisaidia kumvalisha glavu mmoja wa wanakikundi cha kufuga nyuki
Kikundi cha ufugaji nyuki katika mavazi rasmi ya kujikinga na nyuki mbele ya wananchi wa kijiji cha Ludilo
No comments:
Post a Comment