Timu
ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT) imegawa vifaa vya
ufugaji nyuki katika vijiji ambayo vinatekeleza mradi wa Ushiriki wa Wananchi
katika Usimamizi wa Maliasili, unaofadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). Mradi huu unatelekezwa
katika vijiji 32 vya wilaya za Iringa na Mufindi, mkoani Iringa.
Mradi
wa ufugaji nyuki unalenga kusaidia jamii zilizozungukwa na rasilimali misitu na
wanyamapori, kujipatia kipato mbadala ilikupunguza utegemezi wa kipato
unaotokana na maliasili zilizo wazunguka.
Mradi
wa ufugaji nyuki umelenga kuwafikia wananchi 700, kwa kupatiwa mafunzo ya
ufugaji nyuki pamoja na kupewa mizinga na vifaa vya ufugaji nyuki. Kila
mwananchi aliyepatiwa mafunzo hayo, hupewa mzinga mmoja na vifaa, ikiwemo
kofia, wavu wa kuzuia kuumwa na nyuki, suti, glavu na viatu maalum.
Vifaa
vya ufugaji nyuki na mizinga hugawiwa kwa awamu tofauti, kwa awamu hii jumla ya
vijiji nane vimefikiwa. Vijiji hivyo ni Malinzanga, Kiwere,Mfyome, Kitapilimwa,
Itagutwa, Tungamalenga, Kitisi na Idodi.
Afisa Ugani wa LEAT Hna Lupemba (kulia) akigawa vifaa vya uafugaji nyuki kwa wanakikundi wa kijiji cha Tungamalenga, wilayani Iringa
Mmoja wa wanakikundi caha ufugaji nyuki wa Tungamalenga akisaidia kumvalisha mwenyekiti wa kijiji
Mwenyekiti wa kijiji cha Tungamalenga akiwa katika mavazi ya ufugaji nyuki
Baadhi ya vifaa vya ufugaji nyuki vilivyo gawiwa kwa wanakikukndi, kijijini Tungamalenga
No comments:
Post a Comment