Wednesday, May 11, 2016

WANANCHI WA KIJIJI CHA MWITIKILWA WAJIPANGA UFUGAJI NYUKI


 Kikundi cha wafugaji nyuki cha kijiji cha Mwitikilwa cha wilaya ya Mufindi chajipanga kuzalisha asali kwa wingi ilikukidhi mahitaji katika jamii.
Kikundi hicho cha watu 22 kilihudhuria mafunzo ya siku tatu mahususi kwa ufugaji bora na wenye tija. Baada ya mafunzo kikundi kilipatiwa vitendea kazi, vikiwemo suti, glavu, kofia, wavu wa kujikinga uso, viatu, patasi na nta.

 Mafunzo ya ufugaji nyuki ni sehemeu ya utekelezaji wa mradi wa 'Ushiriki wa Wananachi katika Usimamizi wa Maliasili' mradi unaotekelezwa na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa ufadhili wa watu wa Marekani, kupitia shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). Mradi unatekelezwa katika vijiji 32 vya wilaya mbili za mkoa wa Iringa, wilaya ya Mufindi na Iringa.

 Lengo la mafunzo ya ufugaji nyuki ni kusaidia jamii zinazoishi karibu na rasilimali misitu na wanyamapori, kuinua uchumi wao bila ya kutegemea zaidi katika rasilimali zinazo wazunguka. Rasilimali ambazo ni chache na zinazo hitaji kutunzwa vizuri kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.

Mafunzo haya yalitolewa na Afisa Nyuki wa wilaya ya Mufindi, Hamis Hassan, na Thomas Mtelega wa Asasi ya ASH-TECH ambao ni washiriki wa utelekezaji wa mradi.

Wanakikundi cha ufugaji nyuki wakifuatilia mafunzo kutoka kwa Afisa Nyuki wa Wilaya ya Mufindi bwana Hamis Hassan (Hayupo pichani)


Baadhi ya wanakikundi cha ufugaji nyuki wakiwa na Afisa Nyuki wa Wilaya ya Mufindi bwana Hamis Hassan (wa kwanza kushoto mstari wa mbele-mwenye koti la bluu bahari bila kofia)

 

No comments:

Post a Comment