Wadau
wa Mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili Waipongeza LEAT
Wadau wa mradi wa Ushiriki wa wananchi katika Usimamizi
wa Maliasili waipongeza Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo,
kwa kutekeleza shughuli za mradi kwa kushirikisha wadau wote muhimu.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa alisema haya………
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tathmini
ya maendeleo ya mradi kwa kipindi cha miezi sita, kuanzia Novemba 2015 hadi
Aprili 2016, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mheshimiwa Richard Kasesela, alisema
taasisi ya LEAT imefanikiwa katika utekelezaji za mradi wake kwasababu ya
utaratibu mzuri waliojiwekea, ikiwemo kushirikisha wadau mbalimbali ikiwa ni
pamoja na Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Halmashauri za Wilaya, Serikali za vijiji, Mashirika
ya kijamii, wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Alisema’ LEAT imepokelewa vizuri na wananchi wa
Iringa kwasababu walitambua umuhimu wa kushirikisha wadau wote toka kuanza kwa
mradi hivyo wananchi wanauthamini mradi na kuona kuwa wao ni sehemu ya
mafanikio ya mradi’.
Alifafanua kuwa mafaniko ya mradi wa LEAT ni pamoja
na mwitikio mkubwa wa wananchi kushiriki katika usimamizi wa maliasili, kwa
kutoa taarifa za uhujumu maliasili unaoendana sambamba na ukamataji wa
rasilimali za misitu.
Mkuu wa Wilaya alitolea mfano, wananchi walivyoweza
kukamata mbao 298 mwezi Januari 2016, katika kijiji cha Mfyome, na mbao 491
zilizokamatwa katika kijiji cha Tungamalenga wilayani Iringa.
Pia alipendekeza LEAT na waandishi wa habari
waanzishe ukurasa katika mitandao ya kijamii kwaajili ya kuwaripoti waharibifu
wa mazingira, ikiwa ni Pamoja na kuweka picha zao katika kurasa hizo. Alisema kutokana
na kasi kubwa ya uvunaji miti, ipo haja ya wadau wote kuanzisha kampeni ya
kutokomeza uvunaji haramu kama inavyofanyika kampeni ya kuzuia mauaji ya tembo.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Iringa Alonga…..
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Hamlashauri ya Iringa
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Halmashauri za Iringa, Mheshimiwa
Steven Mhapa alisema kuwa miradi mingi iliyotekelezwa mkoani Iringa haikuweza
kuendelezwa kwasababu serikali na wananchi hawakushirikishwa kikamilifu kuanzia
katika hatua za awali za mradi, hivyo wadau hao huhisi kuwa wao sio muhimu
katika kufikia malengo ya mradi.
Aliye simama ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Mkoa wa Iringa, Mh. Steven Mhapa
“Nawapongeza
LEAT kwakuwa wanafahamu umuhimu wa wadau wote katika kufikia malengo ya mradi,
walishirikisha ofisi ya Wakuu wa Wilaya, Halmashauri na wananchi, ndio maana
hata leo hii tumejumuika nao katika mkutano wa tathmini ya mradi, kwa kuwa na
sisi ni sehemeu ya mafanikio ya mradi.
Mheshimiwa Mhapa alitoa angalizo kuwa kutokana na
umuhimu wa maliasili katika ustawi wa uchumi wa nchi,LEAT iangalie namna
itakavyoweza kuongeza wigo wa mradi katika wilaya nyingine za mkoa wa Iringa,
ili wananchi waliozungukwa na maliasili wafahamu thamani ya rasilimali misitu
hususan mbao. Alisema serilkali za vijiji vinvyozungukwa na rasilimali misitu zinapokea
mapato hafifu ambayo hayalingani na thamani ya miti inayovunwa.
Tutaendelea
kushirikiana na LEAT-Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi
Mheshimiwa Ashery Mtono,
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi alisema kuwa halmashauri yake itaendelea
kushirikiana na LEAT kwakuwa wameona mafanikio ya mradi katika halmashauri
yake. Alisema wananchi wamepata mwamko mkubwa kuhusu ushiriki waa katika
usimamizi wa maliasili, kuwa matukio ya ukamataji wahujumu maliasili
yameongezeka, pia wananchi wamepata ujasiri wa kuhoji viongozi wao juu ya mapato
na matumizi ya maliasili. Pia wananchi wana ujasiri wa kudai uwazi na
uwajibikaji kutoka kwa viongozi wao, hivyo kuboresha utoaji wa huduma za jamii.
Mkurugenzi
Mtendaji wa LEAT aelezea lengo la mkutano wa tathmini ya mradi
Akizungumza katika
mkutano wa tathmini ya mradi kwa kipindi cha miezi sita, Novemba 2015 hadi
Aprili 2016, Mkurugenzi Mtendaji wa Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira
kwa Vitendo (LEAT), Dkt. Rugemeleza Nshala alisema kuwa lengo la mkutano
ilikuwa kupima utekelezaji wa mradi, kwa kuangalia mafanikio, changamoto na
mipango ijayo ilikuhakikisha kuwa wadau wote kila mmoja kwa nafasi yake
anashiriki kikamilifu ilikufikia malengo ya mradi.
Mkurugenzi Mtendaji wa LEAT, Dkt. Rugemeleza Nshala akiwasilisha taarifa ya jumla ya maendeleo ya mradi
Afisa Mradi Mwandamizi, Remmy Lema, akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi
Timu ya LEAT: Kutoka kushoto: Hadija Mrisho, Glory Kilawe, Edina Tibaijuka na Glory Ephraem
Pia aliwashukuru
viongozi wa Wilaya na Halmashauri za Iringa na Mufindi kwa kushiriki bila kuchoka
tangu kuanza kwa mradi mwaka 2014 mpaka sasa.Pia aliwajulisha wadau kuwa
milango ya LEAT ipo wazi ilikutoa fursa kwa wadau wote kutoa mchango ya
kuboresha utekelezaji wa mradi.
LEAT
imeboresha utendaji wake -Mwakilishi kutoka Chemonics
Mwakilishi kutoka
shirika la Chemonics, Thobias Chelechele, ambao ni Wakala wa Shirika la
Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID-Wafadhili wa mradi), aliipongeza LEAT
kwa kuboresha utendaji wake, na kuwa hiyo ni kiashiria cha kufanikiwa kwa
mradi.
Bwana Thobia,pia
alizishauri Asasi za kiraia kuhakikisha kuwa wanafuata miongozo ya uendeshaji
shirika ikiwemo masuala ya utawala, fedha, utunzaji kumbukumbu na utekelezaji
mradi kwa ujumla, iliwaweze kukua na kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata fedha
baada ya mradi huu kwisha.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau kutoka wilaya za
Iringa na Mufindi, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Wenyeviti wa halmashauri,
Wakuu wa idara za maliasili, Waruzuku wa mradi, asasi za kiraia na wananchi.
Mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa
Maliasili unatekelezwa katika wilaya za Iringa na Mufindi, mkoani Iringa. Mradi
huu umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID), na
unatekelezwa na Timua ya Wanansheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT)
kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia.
Asasi
za Kiraia wapatiwa Vitendea Kazi
Asasi za Kiraia ambazo pia ni watekelezaji wa mradi
wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, wapatiwa kompyuta
mpakato (laptop) ilikurahisisha utendaji wa shuguli zao. Asasi za Kiraia
zilizopokea kompyuta mpakato ni MBOMIPA, MUVIMA, ASH-TECH na MJUMIKK.
Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia ya ASH-TECH, Erasto Mazera akipokea kopmyuta mpakato kwaajili ya kurahisisha utekelezaji wa mradi
Mwenyekiti wa MBOMIP akipokea kompyuta mpakato
Mwenyekiti wa Asasi ya MJUMIKK, Mashaka Kilanga akipokea kompyuta mpakato
Mkurugenzi wa MUVIMA akipoke kompyuta mpakato
Bwana Komba akiwasilisha sehemu ya utekelezaji ya asasi yake ya MJUMIKK
Sehemu ya Wadau wakifuatilia mawasilisho kutoka kwa watekelezaji mbalimbali wa mradi
Wadau wa mradi wakifuatilia mawasilisho ya maendeleo ya maradi
No comments:
Post a Comment