Saturday, May 21, 2016

KIKUNDI CHA UFUGAJI NYUKI CHA KIJIJI CHA IHEFU WILAYA YA MUFINDI WAHITIMU MAFUNZO

Timu ya watu 22 wa kikundi cha ufugaji nyuki katika kijiji cha Ihefu wilayani Mufindi, wahitimu mafunzo ya siku tatu ya ufugaji nyuki.
Mafunzo hayo ambayo hutolewa na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo(LEAT) yanalenga kuwezesha wananchi kuanzisha shughuli mbadala za kuongezea kipato katika vijiji 32 vinavyotekeleza mradi wa 'Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili' ...unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). 

 Katika awamu ya kwanza ya mafunzo ya ufugaji nyuki wanakikundi walijifunza umuhimu wa asali kwa matumizi ya kila siku, aina za nyuki, ufugaji bora, jinsi ya kutundika mizinga na uvunaji bora.

Awamu ya pili ya mafunzo itahusu usindikaji na jinsi ya kutafuta masoko ndani na nje ya nchi.
Baada ya kuhitimu mafunzo kila mshiriki alipewa vitendea kazi ambavyo ni mzinga wa nyuki, nta, patasi na vifaa vya kujikinga na nyuki- kofia, wavu wa kuzuia uso, glavu, suti na viatu maalum.
Mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili unatekelezwa katika vijiji 32 vya wilaya za Iringa na Mufindi katika mkoa wa Iringa.

 Wilaya hizo zilichaguliwa kwasababu zina maeneo ya usimamizi wa wanyamapori, rasilimali za wanyamapori, misitu na maeneo ya hifadhi. Lengo kuu la mradi ni kuhakikisha kuwa wananchi wanashiriki kikamilifu katika usimamizi wa maliasili.
Pia kutetea usimamizi bora wa maliasili ilikupunguza umasikini na kuhakikisha uhifadhi endelevu wa uhainuai, kuiwezesha jamii kuwa na utamaduni wa ushiriki katika masuala yanayohusu maliasili, kuzijengea uwezo jamii za wenyeji uwezo wa katika kuziwajibisha na kuzisimamia taasisi za serikali zenye majukumu ya kuhifadhi na kusimamia maliasili.
Sehemu ya wanakikundi cha ufugaji nyuki wakiwa darasani


Baadhi ya wanakikundi cha ufugaji nyuki wakiwa katika mavazi ya kujikinga na nyuki

Wanakikundi cha ufugaji nyuki wakifuatilia mafunzo
 
 

No comments:

Post a Comment