Friday, May 13, 2016

MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MALIASILI KATIKA KIJIJI CHA KINYIKA-WILAYA YA IRINGA

Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa kushirikiana na Asasi ya MBOMIPA ambao ni watekelezaji wenza katika mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, wamehitimisha mafunzo ya siku saba katika kijiji cha Kinyika, wilaya ya Iringa.

 Kijiji cha kinyika ni moja ya vijiji vilivyopo katika eneo la Usimamizi wa Wanyamapori linalosimamiwa na Asasi ya MBOMIPA, hivyo mafunzo hayo ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wa maeneo hayo; wanafahamu haki yao ya kikatiba katika kusimamia rasilimali misitu na wanyamapori kwa maendeleo endelevu ya kizazi cha sasa na kijacho.

 Hapa nchini na maeneo mengine duniani, kumezuka wimbi la watu wachache kuvuna rasilimali misitu na wanayamapori kwa manufaa binfsi ambayo si rafiki kiuchumi na kimazingira. Tumeshuhudia wanyapori wakiuawa kwa kasi sana na hasa tembo, simba na chui.

Pia katika sekta ya misitu tumeshuhudia uvunaji haramu na usio endelevu unao hatarisha hatma ya kizazi hiki.
Mafunzo hayo yalihusu mambo muhimu katika usimamizi dumivu wa misitu na wanyamapori, kwa kuangalia sera na sheria zinasema nini katika kusimamia rasilimali hizo. Pia, washiriki waliangalia miongozo, kanuni na adhabu, ambazo zitawasaidia katika kutengeneza sheria ndogondogo za vijiji za usimamizi wa maliasili.

Mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili umefadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). Mradi unatekelezwa katika vijiji 32 vya wilaya za Iringa na Mufindi, mkoani Iringa.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo wakijibu maswali ya awali kabla ya mafunzo, ilikupima wanaelewa kiasigani dhana ya Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa maliasili
 
 
 
Washiriki wa mafunzo katika kazi za vikundi
 
Afisa Ugani wa LEAT, Hana Lupembe (aliye vaa gauni jekundu) katika piacha ya pamoja na Washiriki wa mafunzo

No comments:

Post a Comment