·
Tangu
mwaka 1949 Bonde la Msimbazi lilitangazwa kuwa eneo hatarishi
·
Zoezi la
ubomoaji liataendeshwa kwa utaratibu mzuri
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, January Makamba |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba
alisema kuwa waliovamia mabondeni wataondolewa na hawatalipwa stahiki yoyote
kwa kuwa wamevunja sheria. Makamba alisema kuwa utaratibu huo ulikuwepo katika
awamu nne za Marais waliotangulia, tatizo utekelezaji wa sharia haukufuatwa
kikamilifu.
Alisema kuwa bonde la Msimbazi lilitangazwa kuwa eneo
hatarishi kwa maisha ya watu tangu mwaka 1949 na baadaye mwaka 1979. “Kumekuwa
na taratibu za kuondoa watu ilikurejesha maeneo hayo katika hali yake ya asili”,
alisema.
Aliongeza kuwa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi
iliwahi kutangaza Bonde la Msimbazi kuwa eneo maalum na mipango miji,
ilikutimiza suala hilo ilikuwa lazima watu waondolewe.
Alisema kazi ya kuwaondoa wananchi wanaoishi kwenye bonde
hilo ilikumbwa na changamoto kadhaa na kukajengeka dhana kuwa wanaonewa.
“Serikali tulieleza kama mtu alipewa kibali na serikali
akajenga nyumba, basi serikali ilifanyamakosa na itamtafutia mahali pengine.
Ila kama mtu alikuja tu na kujenga nyumba eneo hilo, lazima aondoke”, alisema
Makamba.
Alifafanua kuwa waliovamia na kujenga mabondeni serikali
haiwezi kuweka utaratibu wa kuwapatia maeneo mengine kwa sababu kufanya hivyo
ni sawasawa na kuwapa zawadi wanaovunja sheria. Aliongeza kuwa licha ya watu
kujenga nyumba na kufikia kiwango cha kuishi, haiwezi kuwa kipimo cha
kujipambanua kuwa hawana makossa.
“Unapofanya makossa ukamilifu wa kosa siyo msamaha wa kutorekebishwa.
Ukisema kwasababu mtu hakukamatwa wakati akijenga msingi basi asikamatwe
kwasababu nyumba imeisha si kweli”, alisema.
Alisema kazi ya kubomoa nyumba zilizo mabondeni iliingiliwa
na wanasiasa na akasisitiza kuwa maisha wanayoishi wananchi katika maeneo hayo,
si ya kuridhisha na ukiwa kiongozi huwezi kukubali kuona wakiendelea kuishi
humo.
“Sisi ambacho tumekubali lazima tuendeleze zoezi lile kwa
utaratibu mzuri zaidi. Lazima watu wapate taarifa na waliovamia kuelezwa wazi
kuwa hawatapata stahiki yoyote na waliopewa vibali na serikali wapewe maeneo
mengine”, alisema Makamba.
“Kuna utamaduni ulijengeka muda mrefu wa watu kutoheshimu na
kutii sharia. Sasa tukiendelea hivyo hivyo si sawa maana bila sharia hakuna serikali.
Nchi hii mtu hawezi kuamua ajenge kibanda mahali popote na akiondolewa serikali
ndiyo ioenkane ina dhambi. Hatuwezi kuendesha nchi kwa utaratibu huu”.
JICHO LA PILI
Zoezi la ubomoaji wa nyumba zilizo jengwa mabondeni limeonekana kuwa
ni uonevu mkubwa kwa wananchi waliojenga katika maeneo hayo. Watu mbalimbali
wakiwemo wanasiasa waliliongelea kwa hisia kali na kuelekeza lawama kwa
serikali. Wakidai kuwa serikali ilikuwa
wapi wakati wananchi hao walipoanza ujenzi katika huko mabondeni.
Inawezekana serikali haikuliona hilo ama kwa namna yoyote
ambayo watu wanaweza kutafsiri, lakini linapojadiliwa suala la sheria
tunaambiwa Kutojua Sheria Si sababu ya Kuvunja Sheria. Kwa uhalisia ukiangalia
masiha ya watu wanaoishi mabondeni ni magumu na hatari mno, kimazingira na
kiafya.
Mabondeni hakuna mfumo mzuri wa uhifadhi taka pamoja na
miundombinu ya kupitisha maji taka, hii ni kutokana na eneo jografia ya eneo ilivyo, wakazi
wa Dar es Salaam wanaelewa hilo. Ingawa kuna watakao hoji mbona hata watu ambao
hawaishi mabondeni wanatatizo la miundo mbinu ya kuhifadhi taka na mirefeji ya
kupitisha maji.
Ni kweli kwa Jiji la Dar Es Salaam kuna tatizo la miundo
mbinu, lakini hali huwa mbaya zaidi kwa wakazi wa mabondeni. Kwa mfano wakazi
wa bonde la Msimbazi wakati wa mvua bonde hujaa maji kiasi kwamba wakazi hao
hulazimika kuhama makazi yao katika kipindi chote cha mvua.
Katika kipindi cha mvua mafuriko ya bonde la Msimbazi yamegharimu
maisha ya wengi na kusababisha hasara za mali za watu. Zaidi ya hayo, wakati wa
mvua watu wengi hutirirsha maji taka kutoka katika majumba yao na kuelekeza
sehemu za mabondeni, hivyo kuhatarisha afya za watu waishio mabondeni.
Ni heri kuchukua tahadhari kuliko kusubiri hatari.
No comments:
Post a Comment