Chanzo: Gazeti la
Raia Tanzania, Machi 1, 2016
Kibaha: Mahakama
ya Hakimu Mkazi mkoa wa Pwani imemuhukumu mfanyabiashara Anania Betela (30)
amehukumiwa kwenda jela miaka 20 na kulipa faini ya Sh.1.9 bilioni baada ya
kupatikana na hatia katika kesi ya kukutwana vipande 28 vya meno ya tembo bila
kibali.
Picha ya Tembo wakiwa katika moja ya mbuga za wanyama za Tanzania |
Mshtakiwa huyo alihukumiwa terehe 29 Februari 2016,
mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Herieth Mwailolo, aliyekuwa akisikiliza
kesi hiyo huku upande wa mashtaka ukiwakilisha na Wakili wa Serikali, Salim
Msemo.
Akitoa adhabu hiyo Hakimu alisema, mshtakiwa alikuwa
akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba moja ya mwaka 2014.
Katika kesi hiyo mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa mwaka 2014
eneo la Vigwaza, wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani ambapo alikutwa na vipande
hivyo vya meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi milioni 198.
Upande wa mashtaka ulikuwa na jumla ya mashahidi watano
Pamoja na vielelezo mbalimbali ikiwemo men ohayo, begi lililobeba meno hayo
katika kuthibitisha kesi dhidi ya mshtakiwa.Baadhi ya meno ya Tembo yaliyo wahi kukamatwa kutokana na ujangili |
JICHO LA PILI
Ujangili unapaswa kupigwa vita, wananchi tunawajibu wa
kuhakikisha kuwa tunasimamia na kulinda rasilimali za Taifa kwa ajili ya
maendeleo yetu na vizazi vijavyo. Vitendo hivi vimekithiri na vinalisababishia
taifa hasara kubwa, ni biashara inayo nufauisha watu wachache. Hebu tujiulize
uvunaji huu wa kasi wa tembo, usipo pingwa, baada ya miaka kumi hali itakuwaje?
Je, kutakuwa na tembo hata mmoja? Vipi kuhusu biashara ya
utalii, itakuwepo?
Ripoti ya Taasisi ya Kulinda Tembo (TEPS) ya mwaka 2015
inaonesha kuwa asilimia 60 ya Tembo waliuawa kuanzaia mwaka 2009 mpaka mwaka
2014. Mwaka 2009 kulikuwa na Tembo 109,051 na ni Tembo 43,330 ndio waliokuwa
wamesalia hadi mwaka 2014. Pia ripoti inaonesha kuwa tembo 61,720 waluiawa kwa
miaka mitano mfululizo ikiwa ni wastani wa Tembo 30 kwa siku.
Ukweli ni kwamba Tembo hao wakiwa hai wanaliongezea taifa
mapato makubwa kupitia biashara ya utalii kuliko wanapo uawa na kuuza meno yao.
Idadi ya Watalii imekuwa ikiongezeka kila mwaka hii
inaonesha kuwa sekta ya utalii inakua na kukuza uchumi wanchi hivyo kila
mwananchi ana wajibu wa kupinga ujangili wa wanyamapori wetu.
Pinga Ujangili, Okoa
Tembo wa Tanzania!
No comments:
Post a Comment