Serikali imewaagiza wataalamu wa upimaji wa kemikali
wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na wale wa SGS katika mgodi wa North Mara,
kuchukua sampuli ya maji yanayo lalamikiwa na wananchi wa Nyamongo kuwa yana
kemikali zenye sumu na kuwa sababishia madhara.
Timu hiyo ya wataalamu kutoka mashirika hayo,
imepewa jukumu hilo kutokana na majibu ya ‘mkanganyo’ aliyopewa Naibu Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhanga Mpina, baada ya
kutembelea mgodi huo wiki mbili zilizopita.
“Serikali imeamua kuwa chukua wataalamu hawa na
Mkemia Mkuu wa serikali ili wayapime maji yaliyo chukuliwa sehemu yenye bwawa
la kutunzia maji machafu, kwani inadaiwa yanapo tiririka nje ya mgodi huwa
letea madhara wananchi”, alisema Mpina.
Aidha mpina aliwataka wananchi wawe na Imani na
wataalamu hao kwa kazi watakayo fanya kutokana na serikali kuamua kuliangalia
tatizo hilo ilikuhakikisha wananchi wake wanaishi kwenye mazingira salama.
Baadhi ya wananchi walioshuhudia uchukuaji wa
sampuli ya maji hayo, walimuomba Mpina kuhakikisha kuwa haufanyiki mchezo
mchafu katika upimaji kwani wao walisha chukua maji hayo yanayo wadhuru na
kuyapeleka Nairobi nchini Kenya kwa vipimo, yaka bainika yana kemikali za sumu.
Naye Afisa wa Uhakiki wa TBS, Julieth Elibariki,
alisema kinachotakiwa kupimwa ni maji na matokeo ya vipimo vine vya kitaalamu
vinavyo julikana ‘micrology chemical paramenters, ‘organic compounds na
contaminats’ huku matokeo ya vipimo hivyo yatachukua siku tano hadi saba
ilikujulikana kama yana kemikali za sumu au vinginevyo.
KUMBUKUMBU YA TUKIO KAMA HILO
Siku ya Ijumaa tarehe 25 mwezi Aprili 2011, blog yetu
iliwahi kutoa taarifa za baadhi ya wananchi wa Nyamongo ambako mgodi wa North
Mara unaendesha shughuli zake, kuwa walipata madhara kutokana na maji yanayo
tiririka kutoka mgodini kudaiwa kuwa na sumu.
Picha hapo chini zinaonesha baadhi ya wananchi walio
athiriwa na maji hayo.
Pia jamii isisahau hata kidogo kile kilichotokea
mwaka 2009, ambapo kemicali-sumu aina ya CYANIDE
ilivuja na kuchanganyikana na maji
yamto THIGITE, mto
unaotumiwa na wanakijiji wa Nyamongo kama chanzo kikuu cha maji ya matumizi ya
kila siku. Kutokana na tukio hilo, inakadiriwa watu wapatao Arobaini (40)
walipoteza maisha, mamia wakiachwa na ulemavu wa kudumu na mifugo zaidi ya Mia
Tano (500) ilikufa kutokana na kutumia maji yaliyochanganyikana na
kemikali hiyo yenye sumu
No comments:
Post a Comment