Wakulima wa mbogamboga jijini Dar Es Salaam wamesema
kuwa hawana njia mbadala ya kutumia maji taka kumwagilia bustani zao kwakuwa
hawapati maji safi kwaajili ya umwagiliaji.
Wakulima waliyasema hayo wakati wa mahojiano na
mwandishi wa gazeti la The Guradian, tarehe 02/02/2016. Walisema kuwa wame elekeza
katika bustani zao mifereji inayo tiririsha majitaka kutoka katika makazi ya
watu. Walisisitiza kuwa iwapo maji safi kutoka katika mabomba au visima
yangekuwa yanapatikana kwa urahisi wangetumia hayo badala ya kutumia maji taka.
Tarehe 02/02/2016 gazeti la The Guradian lilishapisha
katika ukurasa wake wa mbele kuwa Mamlaka ya Uthibiti Anfya nchini imeonya kuwa
watu waishio katika majiji na mijini wanao
kula mboga zinazolimwa katika bustani za mijini wapo katika hatari ya kiafya
ikiwemo kupata maradhi yasiyo tibika.
Wakitoa angalizo hilo kwa Pamoja Mamlaka ya Chakula
na Dawa na Taasisi ya Chakula na Lishe walisema matumiza ya maji taka kwenye
mazao ya mboga za majani na matunda, kachumbari na matunda huwa na bakteria ambao huingia
katika tumbo la binadamu na kusababisha magonjwa kama vile saratani, ugonjwa wa
figo na kuathiri mfumo wa fahamu kwa watoto.
Kwa mujibu wa bwana Edward Melkion ambaye amekuwa
akilima mboga za majani katika bonde Msimbazi tangu mwaka 1991, yeye Pamoja na
wenzake wameelekza katika vitalu vyao mrefeji wa maji taka unaotirirsha maji
kutoka Buguruni, kwa kisingizio cha kukosa maji safi kwaajili ya umwagiliaji.
Akitoa angalizo Mtafiti wa Mafunzo Lishe wa Taasisi ya Chakula na Lishe, bwana
Walbert Mgeni alisema bakteria wanao patikana katika mboga za majani
hufa iwapo
mboga zitapikwa kwa muda mrefu lakini kemikali kama vile madini ya chuma katika
mboga hayapotei bali huingia mwilini.
Sehemu ya bustani zinazolimwa katika bonde la Msimbazi Dar Es Salaam
Sehemu ya bustani ya nyanya iliyopo katika eneo la bonde la Msimbazi, Dar Es Salaam
hufa iwapo mboga zitapikwa kwa muda mrefu lakini kemikali kama vile madini ya chuma katika mboga hayapotei bali huingia mwilini.
Sehemu ya bustani zinazolimwa katika bonde la Msimbazi Dar Es Salaam |
Sehemu ya bustani ya nyanya iliyopo katika eneo la bonde la Msimbazi, Dar Es Salaam |
No comments:
Post a Comment