Thursday, February 25, 2016

MAREKANI YATANGAZA VIVUTIO NGORONGORO

Chanzo: Gazeti la Mwananchi, Alhamis, Februari 25,2016

Ngorongoro: Kituo cha Televisheni cha Marekani cha ABC juzi jumanne kilirusha matangazo ya moja kwa moja kwa saa tatu kuonesha vivutio vya utalii katika Hifadhi ya Ngorongoro iliyopo katika mkoa wa Arusha.
Matangazo hayo ambayo yalionekana katika kituo cha Good morning America, yalirushwa kuanzia saa moja asubuhi hadi saa tatu asubuhi, kwa muda wa Marekani wakati Tanzania ilikuwa saa tisa alasiri hadi saa kumi na moja jioni.
Meneja Mwandamizi Mwendeshaji wa vipindi katika kituo cha ABC, Faruna Sanoon, alisema kituo hicho kimejitolea kuandaa kipindi hicho nchini na baadaye watakwenda Afrika Kusini ilikuonesha utajiri wa vivutio vya barani Afrika.
Alisema kituo hicho kitafanya marudio ya kipindi hicho mara 14 kama walivyoombwa na serikali ya Tanzania.
Akizungumza na Waandishi wa habari mjini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini, Devota Mdachi, alisema matangazo hayo yanatarajiwa kuongeza idadi ya Watalii nchini.
Mdachi alisema matangazo hayo ni jitihada ya serikali kupitia ubalozi wa Tanzania Marekani, ilikuhakikisha Watalii wanaongezeka nchini na kuinua pato la taifa.

Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori, Herman Kerariyo ambaye alimwakilisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema matangazo hayo yanatarajiwa kuongeza Watalii katika Hifadhi ya Ngorongoro kutoka 600,000 kwa mwaka hadi kufikia 1,000,000.
"Kama mnavyoona maeneo mengi duniani kupitia kituo cah ABC na vingine wanaona matangazo ya Ngorongoro, serikali inaamini Tanzania itanufaika sana", alisema.
Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Dk. Fred Manongi, alisema matangazo hayo yametolewa bure na kama Tanzania ingelipa ingepaswa kutoa dola milioni 250 za Marekani.
Alisema licha ya kuonesha wanyamapori pia wameonesha, utalii na utamaduni unaopatikana katika hifadhi hiyo.
"Eneo hili ni la pekee duniani kwani wanyamapori na binadamu wanaishi sehemu moja, bila ya matatizo, hatua inayofanya hifadhi hiyo kuwa moja ya maajabu saba ya asili barani Afrika, na eneo maalum la uhifadhi duniani, alisema.
Pundmilia katika Hifadhi ya Ngorongoro
 
Boma la Wamasai lililopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro
 
 
Pundamilia na Simba katika hifadhi ya Ngorongoro

Wednesday, February 24, 2016

WANAKIJIJI WAKAMATA MBAO ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 9

Bwana Chuki Mduda akiwa amesimama mbele ya mzigo wa mbao 298, zilizo vunwa bila kibali, mbao hizo zilivunwa katika msitu wa asili wa Gangalamtumba katika kijiji cha Mfyome


Wananchi wa kijiji cha Mfyome kata ya Kiwere, katika halmashauri ya Iringa Vijijini wamekamata mzigo wa mbao 298 zilizo vunwa isivyo halali katika msitu wa asili wa Gangalamtumba, hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira.

Ukamatwaji wa mbao hizo ni matokeo ya mafunzo ya mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, maradi unaotekelezwa na Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Mwishoni mwa mwezi Januari wananchi wa kijiji hicho walikamata mbao hizo, mtuhumiwa alikimbia na kutelekeza mzigo huo. Viongozi wa kijiji waliamua kutaifisha mbao hizo na kuelekeza kuwa zitatumika kutengeneza madawati ilikukabiliana na changamoto ya upungufu wa madawati inayoikabili jamii hiyo.

Kwa upande wake Mjumbe wa Timu ya Ufuatiliaji Uwajibikaji katika Jamii kwa ngazi ya Wilaya, ambaye ni mkazi wa kijiji hicho bwana Chuki Mduda alisema kuwa mafunzo ya Ushiriki wa Wananchi katika Usimamaizi wa Maliasili yameleta hamasa na mwamko mkubwa katika jamii kwakuwa wananchi sasa wananshiriki kikamilifu na matokeo ya kukamatwa kwa mbao hizo ni kielelezo cha ari ya uwajibikaji.

Alisema mbao hizo zilivunwa kutoka katika msitu wa asili wa Gangalamtumba, alidai kuwa tayari eneo kubwa la msitu huo limeathiriwa vibaya.

“Tangu tulipohudhuria mafunzo haya kumekuwa na mabadiliko makubwa, tume hamasika kulinda maliasili zetu, na tumejipanga kupambana na wote watakao vuna rasilimali misitu bila ya kibali, tutawachukulia hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kuwanyang’anya rasilimali watakazo kamatwa nazo na watalipa faini kulingana na sheria za kijiji”, alisema Mduda.


Pope Francis Adviser calls on Florida Polls to Address Climate Change

Source: The Helard of February 24, 2016
Writer: Jenny Staletovitch


MIAMI -- Florida politicians have a duty to address the perils of climate change even if they don't believe humans are hastening its grave consequences, Pope Francis' chief adviser on climate change said in an interview with the Miami Herald before addressing a weekend conference on climate, nature and society at St. Thomas University law school.
Cardinal Peter Turkson said: "Anybody running for public office who sees the life of the people affected by climate-related disasters" needs to act.
 
Cardinal Peter Turkson, Pope Francis's Adviser
That, he said, includes the state's two Republican presidential contenders -- former Gov. Jeb Bush and Sen. Marco Rubio -- who remain skeptical of the science tying climate change to increased carbon emissions.
"You'll not be shocked by this," Turkson added. "I also know of a cardinal or two who don't believe
 
As president of the Pontifical Council for Justice and Peace, which also includes St. Thomas human rights professor Roza Pati, Turkson played a critical role in helping Francis draft the historic encyclical released last year. Leading up to the United Nations Paris talks that ended with a global pact to reduce carbon emissions, the manifest put the pope squarely in the middle of the debate, drawing praise for adding his significant influence to the issue and flack for meddling with what critics called a secular topic.
"One letter to me said the pope is about to turn a lie into a doctrine," said Turkson, who was born in Ghana and, as a member of the Francis's advisory council, is considered a contender to be the next pope. "It's not been smooth sailing in all regards."
While Francis' encyclical was not the first time the church weighed in on climate change -- in a 2009 address to the United Nations, Pope Benedict XVI called for a "responsible stewardship" -- Francis' encyclical laid out a forceful blueprint. Turkson said about a year before it was released last June, Francis "expressed a desire to develop an encyclical" during a "routine" business meeting.
Turkson said a "small draft" was prepared, from which the 192-page encyclical grew. When asked about what the pope personally added, Turkson said church officials preferred not to talk about how church manifests are composed.
"I'll be frank. I myself have resisted taking the draft and looking at it," he said.
Because the issue is so critical, Turkson said church officials decided it was important to extend their message beyond church borders. Bishops around the world were prepped and coached on how to best answer questions from the media. The encyclical was also released a month before the Vatican hosted a conference for mayors from around the globe pledging to support the U.N.'s sustainable development goals to combat climate change as well as poverty, hunger and inequality.
Turkson said the church is also trying to reduce its own carbon footprint and has met with a solar panel manufacturer in Rome. In April, the Vatican is planning an event to talk about the challenges to creating greener businesses.
The encyclical's statement on climate change was an early signal Francis would not be afraid to venture into charged political issues. Most recently, he called Donald Trump's plans to build a wall along the Mexican border "not Christian."
In his St. Thomas address, Turkson reminded his Miami audience the encyclical is meant more as a social contract than climate manifest.
"While those in coastline mansions have the money to move if needed," he said. "The worst suffering will hit the poorest areas where residents are barely getting by."
 
 
 
 
 

Kutana na Salome Choga Mwanamke aliye dhamiria kuongeza kipato kupitia Mradi wa Ufugaji Nyuki


Salome Choga wakati wa mahojiano katika msitu wa kijiji cha Lugoda Lutali, Mufindi, Iringa


Salome Choga ni Mjumbe wa Kamati ya Maliasili ya kijiji cha Lugoda Lutali, wilayani Mufindi, mkoani Iringa. Kijiji hicho ni kati ya vijiji 32 vilivyofikiwa na mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili. Mradi huo unaratibiwa na Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa vitendo, (LEAT), kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani, (USAID).

Katika kipindi chote cha maisha yake, Salome amekuwa akitegemea biashara ndogondogo pamoja na kilimo alicho dai kuwa hakina tija sana, kwakuwa mapato hayakidhi mahitaji ya familia yake. Ana watoto wawili mmoja ana umri wa miaka kumi na nne na mwingine ana miaka kumi wote wanasoma katika shule ya msingi Lugoda Lutali. Kwa muda mrefu Salome ndiye mtafutaji wa kipato kwaajili ya familia baada ya mume wake kuondoka na kuishi mbali na familia.

Salome alipongeza Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT) kwa kuleta mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, uliofadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). “Mradi huu unaleta tija katika jamii kwani licha ya kuwa unafundisha na kuhamisisha jamii kulinda na kusimamia maliasili pia wametuletea mradi wa ufugaji nyuki kama njia mbadala ya mapato, ilikupunguza utegemezi wa mapato kwa kuuza rasilimali zilizopo katika misitu”, alisema.

Ingawa hakushiriki katika mafunzo ya ufugaji nyuki anatarajia kushiriki katika awamu ijayo. Katika kipindi chote cha maisha yake amekuwa akitegemea biashara ndogondogo pamoja na kilimo katika kujipatia mapato ya kuendesha maisha ya familia yake. Alieleza kuwa yeye ni mama wa watoto wawili na ndiye mlezi pekee wa watoto hao hivyo ana jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa anaongeza kipato kwaajili ya kusaidia familia yake. “Kwa muda mrefu sasa mume wangu anaishi mbali na familia, mimi ndiye niliye beba jukumu la kulea watoto wetu kwa kuhakikisha wana pata lishe bora, wana kwenda shule pia wanapata huduma za matibabu wanapokuwa wagonjwa”, alifafanua.

Aliendelea kusema kuwa, mradi wa ufugaji nyuki utasaidia kuongeza kipato na kuboresha maisha ya familia. Ni kweli serikali imetangaza elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, lakini bado kuna gharama za vifaa vya shule, pia ninapenda watoto wangu wasiishie kidato cha nne, natamani kuona watoto wangu wakipata elimu cha chuo kikuu, na haya yote yanahitahitaji fedha. Ni vyema nikaanza sasa kuwekeza kwaajili ya gharama za elimu ya juu.

Kazi ya Ufugaji nyuki hapa kijijini hufanywa na wanaume, hii ni kutokana na ugumu wa shughuli yenyewe. Lakini mafunzo yaliyotolewa na LEAT ya namna bora ya ufugaji nyuki yameondoa woga wa  wanawake walishiriki, kunamwamko mkubwa na utayari wa wanawake kujiunga na vikundi vya ufugaji nyuki. Kazi ya ufugaji nyuki imeonekana kuwa rahisi kutokana na uwepo wa mavazi ya kujikinga na nyuki pamoja na mizinga ambayo inaendelea kugawiwa bure kwa washiriki wote.


Baadhi ya mizinga ya kufugia nyuki iliyo gawiwa kwa wanavikundi vya ufugaji nyuki, kabla ya kutundikwa
 
Kuhusu nafasi ya mwanamke katika usimamizi wa maliasili, alisema amejifunza umuhimu wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda na kusimamia maliasili. Katika hilo, anaona jukumu kubwa alilonalo mwanamke katika usimamizi wa maliasili kwa kuwa mama ndiye mtumiaji mkubwa wa rasilimali hizo na zinapo haribiwa mama ndiye anapata athari kubwa.

Uharibifu wa maliasili huathiri watu wote hata viumbe hai wanao ishi kwa kutegemea uwepo wa maliasili hizi. Alimtaja mama kuwa ndiye anaye athirika zaidi kwa sababu, misitu huhifadhi vyanzo vya maji, hivyo inapo haribiwa vyanzo vya maji hukauka na mwanamke hulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji hivyo hupoteza muda mwingi pia ni hatari kiafya na kiusalama.

Kutokana na athari hizo mwanamke anapaswa awe mstari wa mbele kuhamasisha jamii kushiriki katika usimamizi wa maliasili. Kwa bahati mbaya ushiriki wa wanawake ni mdogo, hii inapunguza uzito wa athari za uharibifu wa maliasili kwa jamii. ‘Kulingana na uzoefu wangu ni kuwa madhara yeyote yanapewa uzito iwapo waathirika wataelezea athari hizo’. Mimi kama mama napaswa kuwajibika kueneza elimu ya ushiriki wa wananchi katika usimamazi wa maliasili, nahasa rasilimali misitu.

'Huwa nahamasisha wananwake wenzangu tunapo kutana katika vikao vyetu, lakini nimepewa changamoto ya kuongeza wigo wa kuhamasisha katika mikutano ya hadhara ya kijiji, ili hata wanaume waelewe ni jinsi gani uharibifu wa maliasili utaathiri wanawake'.

Mimi na wanawake wenzangu tulio pata fursa ya kushiriki mafunzo, tunalo jukumu kubwa la kuhamasisha umuhimu wa jamii kutunza maliasili zilizopo kwasababu maliasili zikiharibiwa kurejesha hali ya awali ni gharama na huchukua muda mrefu, wakati huo jamii ikiendelea kupata taabu.

'Naamini mwanamke ni mtu muhimu katika uhamasishaji wa mambo mbalimbali katika jamii, pia wanawake wakiamua kusimamia jambo mara nyingi huhakikisha kuwa jambo hilo linafanikiwa', alisisitiza.
Jumla ya vikundi 16 vya ufugaji nyuki vimepatiwa mafunzo katika wilaya mbili za Iringa vijijini na Mufindi ambako mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili utatekelezwa. Pi jumla ya mizinga 350 imegawiwa kwa wanavikundi na tayari imekwisha tundikwa. Mizinga 350 ni sawa na asilimia hamsini ya lengo la mradi ambalo ni kugawa mizinga 700, katika kipindi cha mradi.
 
 

 

 


 

Thursday, February 11, 2016

NINE IN COURT FOR MURDER OF CONSERVATIONIST


Source: The Citizen, Thursday, 11, February 2016
Simiyu. Nine people appeared before the Bariadi Resident Magistrate’s Court charged with shooting down a helicopter and killing a British Pilot, Rodgers Gower, 37. They also face charges of economic sabotage and illegal possession of firearms.
The Conservationist, Rodgers Gower
 
The helicopter crashed when it was tracking a group of elephant poachers at Maswa Game Reserve in Meatu district, Simiyu region.
Public Prosecutor Yamiko Mlekano claimed that on January 29, this year the accused persons killed Pilot Gower in Maswa game Reserve, Meatu district, Simiyu region. Before the Principle Magistrate John Nkwabi the Public Prosecutor claimed the first defendant, Iddi Mashaka, 49, coordinated economic sabotage contrary to section 4 (1) (d), 51 (1) and 60 (2) of the Economic Sabotage Act.
He claimed between January 6 and first February, the first accused advised the second accused, Shija Mjikato kill an elephant worth32.8 million.
Other accused are 38, Njile Gunga, 28, Dotto Pangali, 42, and Moses Mndagu, 28, Dotto Huya,45, Mwigulu Kanga,40, Mapolu Njige,50, and Mange Barumi,47 who allegedly organized, coordinate nad carryout the killing of elephants.

It was alleged in court that the accused persons were found in possession of illegal ivory, government trophies weighing 31 kilograms worth 32.8 million.

In murder charges, the Public Prosecutor alleged that Shija Mjika, 38, Njile Gunga, 28, Dotto Pangalli, 42 and Moses Mndago,28, did kill the British Pilot. The accused were not allowed to enter any plea because the court does not have jurisdiction to adjudicate on such cases. The case will be mentioned on February 24.

MAPAMBANO DHIDI YA UJANGILI-Hifadhi, Mbuga Kulindwa Kijeshi


Chanzo: Gazeti la Mwananchi, 10 Februari, 2016

Waziri wa Maliasili an Utalii, Profesa Jumanne Maghembe
 
Wizara ya Maliasili na Utalii imesema inatathmini mbinu za kukabiliana na majangili na itaanzisha jeshi Usu litakalokuwa na jukumu la kupambana na ujangili kwenye mbuga na hifadhi zote nchini.
Mpango huo umetangazwa siku moja baada ya Jeshi la Polisi kukamata watu tisa wanao tuhumiwa kuhusika na utunguaji wa helikopta iliyokuwa ikifanya doria kwenye Pori la Akiba la Maswi na ranchi ya wanyamapori ya Mwiba.

Katika shambulio hilo la Januari 29, Rubani wa helikopta hiyo Rodgers Gower aliuawa na Rubani Msaidizi kujeruhiwa. Mbali na tukio hilo kumekuwa na idadi kubwa ya wanyamapori wanao uawa na majangili, hasa tembo ambao kasi ya kutoweka kwake imestua dunia.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, alisema wizara yake imejipanga kuimarisha pambano dhidi ya ujangili na usafirishaji haramu wa mazao ya wanyamapori na misitu.

Kuhusu waliokamatwa kwa tuhuma za kuangusha helikopta hiyo, alisema watu hao walikamatwa na silaha mbili aina ya riffle pamoja na risasi tano, pikipiki moja na kilo 31 za pembe za ndovu alizodai kuwa walimuua siku ya tukio. Katika wiki hiyo ya msako walikamata majangili wanne katika hifadhi ya Selous wakiwa na silaha 20 na Wilayani Tunduru walipata silaha 400.
Waziri, aliwapongeza wananchi na kuwataka waendelee kushirikiana na mamlaka husika.

Tuesday, February 9, 2016

CHAMA CHA WANASHERIA WATETEZI WA MAZINGIRA WAADHIMISHA MIAKA KUMI YA KIFO CHA VINCENT SHAURI


Marehemu  Vincent Shauri Enzi ya uhai wake.

Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) waadhimisha miaka Kumi ya kifo cha Vincent Shauri, aliye fariki kwa saratani mapafu, tarehe 9 Februari 2006.
Vincent Shauri alikuwa mmoja wa waanzilishi wa LEAT, na aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa LEAT kuanzia Octoba 2003 hadi Februari 2006, alipofikwa na mauti.
Katika kuadhimisha miaka kumi ya kifo cha Vincent Shauri, Mkurugenzi Mtendaji wa LEAT Dr. Rugemeleza Nshala pamoja na wafanyakazi walisimama kwa dakika moja ilikutoa heshima kwa mchango wa Shauri katika asasi hiyo.

Marehemu Shauri alitambulika na kuheshimika kwa mchango mkubwa alio utoa kwa taifa na hata katika jumuiya ya kimataifa. Marehemu Shauri alishiriki katika harakati mbalimbali za utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa maliasili, mchango wake utakumbukwa daima na kuenziwa.

Moja ya harakati alizoweza kuanzisha na kusimamia ni pamoja na kuitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu (kwa sasa unaitwa Bulyanhulu Acacia mine), kutokana na madai ya baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo pamoja na wananchi waliokuwa wakiishi karibu na mgodi kudai kuwa kulikuwa na watu takriban 52 waliozikwa wakiwa hai katika mgodi huo.
Pia alishiriki katika uandishi wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 sheria ambayo inatumika hapa nchi mpaka leo hii. Zaidi ya hayo, mchango wake katika uandishi wa Sheria ya Misitu ya mwaka 2002 utakumbukwa daima.

Kutokana na weledi na mchango wake, Shauri alipata fursa ya kusimamia miradi iliyokuwa ikiendeshwa na mashirika ya kimataifa, kwa mfano, mwaka 1999-2002 ali iwakilisha nchi kama Mshauri na Kiongozi wa Mradi uliokuwa ukiandaa namna ambavyo sheria ya kimataifa itatekelezwa katika kusimamia matumizi ya maji ya ukanda wa Ziwa Nyasa, mradi huo ulitekelezwa na Shirika la Chakula Duniani (FAO).

Mwaka 1998 aliungana na Wataalamu wengine jijini Roma, Italia na kushiriki katika mjadala wa Wataalamu uliokuwa ukitathimini Sheria na Sera ya maji, mradi huo uliendeshwa na Shirika la Chakula Duniani.
Mnamo mwezi Agosti, 1997 alipata fursa ya kufanyakazi kama Mshauri wa Sheria katika kutathimini uwiano kati ya ushiriki wa usimamizi wa maliasili na maendeleo ya uchumi wa jamii, za wananchi waishio katika meneo mbalimbali ya hifadhi za taifa.

Shauri aliteuliwa kuwa Mshauri wa Sheria katika mpango wa udhibiti na utekelezaji wa hifadhi ya mazingira nchini Tanzania, mwaka 1997.
Katika misitu, Shauri alishiriki katika kikosi kazi kilichokuwa kikifanya marekebisho ya sharia ya misitu na nyuki ya Tanzania, kuanzia mwaka 1998 hadi 1999. Mradi huo ulikuwa sehemu ya uasndishi wa muswada wa misitu, mazingira na viumbe hai, ambao uliwasilishwa mwaka 1999.
Hii ni baadhi ya michango yake ambayo itakumbukwa na kuenziwa daima.
Mwenyezi Mungu amrehemu, apumzike kwa amani.

Wednesday, February 3, 2016

HATARI-HATUNA NJIA MBADALA YA MAJI TAKA-WALIMA MBOGAMBOGA WASEMA

 
Wakulima wa mbogamboga jijini Dar Es Salaam wamesema kuwa hawana njia mbadala ya kutumia maji taka kumwagilia bustani zao kwakuwa hawapati maji safi kwaajili ya umwagiliaji.
Wakulima waliyasema hayo wakati wa mahojiano na mwandishi wa gazeti la The Guradian, tarehe 02/02/2016. Walisema kuwa wame elekeza katika bustani zao mifereji inayo tiririsha majitaka kutoka katika makazi ya watu. Walisisitiza kuwa iwapo maji safi kutoka katika mabomba au visima yangekuwa yanapatikana kwa urahisi wangetumia hayo badala ya kutumia maji taka.
 
Tarehe 02/02/2016 gazeti la The Guradian lilishapisha katika ukurasa wake wa mbele kuwa Mamlaka ya Uthibiti Anfya nchini imeonya kuwa watu waishio katika  majiji na mijini wanao kula mboga zinazolimwa katika bustani za mijini wapo katika hatari ya kiafya ikiwemo kupata maradhi yasiyo tibika.
 
Wakitoa angalizo hilo kwa Pamoja Mamlaka ya Chakula na Dawa na Taasisi ya Chakula na Lishe walisema matumiza ya maji taka kwenye mazao ya mboga za majani na matunda, kachumbari na matunda huwa na bakteria ambao huingia katika tumbo la binadamu na kusababisha magonjwa kama vile saratani, ugonjwa wa figo na kuathiri mfumo wa fahamu kwa watoto.
 
Kwa mujibu wa bwana Edward Melkion ambaye amekuwa akilima mboga za majani katika bonde Msimbazi tangu mwaka 1991, yeye Pamoja na wenzake wameelekza katika vitalu vyao mrefeji wa maji taka unaotirirsha maji kutoka Buguruni, kwa kisingizio cha kukosa maji safi kwaajili ya umwagiliaji.
 
 
Akitoa angalizo Mtafiti wa Mafunzo Lishe wa Taasisi ya Chakula na Lishe, bwana Walbert Mgeni alisema bakteria wanao patikana katika mboga za majani
 
hufa iwapo mboga zitapikwa kwa muda mrefu lakini kemikali kama vile madini ya chuma katika mboga hayapotei bali huingia mwilini.
 

Sehemu ya bustani zinazolimwa katika bonde la Msimbazi Dar Es Salaam

Sehemu ya bustani ya nyanya iliyopo katika eneo la bonde la Msimbazi, Dar Es Salaam
 
 
 
 
 
 
 
 

SERIKALI YACHUKUA SAMPULI ZA MAJI MGODI NORTH MARA- Chanzo Gazeti la Nipashe la 02/02/2016


Serikali imewaagiza wataalamu wa upimaji wa kemikali wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na wale wa SGS katika mgodi wa North Mara, kuchukua sampuli ya maji yanayo lalamikiwa na wananchi wa Nyamongo kuwa yana kemikali zenye sumu na kuwa sababishia madhara.

Timu hiyo ya wataalamu kutoka mashirika hayo, imepewa jukumu hilo kutokana na majibu ya ‘mkanganyo’ aliyopewa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhanga Mpina, baada ya kutembelea mgodi huo wiki mbili zilizopita.

“Serikali imeamua kuwa chukua wataalamu hawa na Mkemia Mkuu wa serikali ili wayapime maji yaliyo chukuliwa sehemu yenye bwawa la kutunzia maji machafu, kwani inadaiwa yanapo tiririka nje ya mgodi huwa letea madhara wananchi”, alisema Mpina.

Aidha mpina aliwataka wananchi wawe na Imani na wataalamu hao kwa kazi watakayo fanya kutokana na serikali kuamua kuliangalia tatizo hilo ilikuhakikisha wananchi wake wanaishi kwenye mazingira salama.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia uchukuaji wa sampuli ya maji hayo, walimuomba Mpina kuhakikisha kuwa haufanyiki mchezo mchafu katika upimaji kwani wao walisha chukua maji hayo yanayo wadhuru na kuyapeleka Nairobi nchini Kenya kwa vipimo, yaka bainika yana kemikali za sumu.

Naye Afisa wa Uhakiki wa TBS, Julieth Elibariki, alisema kinachotakiwa kupimwa ni maji na matokeo ya vipimo vine vya kitaalamu vinavyo julikana ‘micrology chemical paramenters, ‘organic compounds na contaminats’ huku matokeo ya vipimo hivyo yatachukua siku tano hadi saba ilikujulikana kama yana kemikali za sumu au vinginevyo.
 
KUMBUKUMBU YA TUKIO KAMA HILO
Siku ya Ijumaa tarehe 25 mwezi Aprili 2011, blog yetu iliwahi kutoa taarifa za baadhi ya wananchi wa Nyamongo ambako mgodi wa North Mara unaendesha shughuli zake, kuwa walipata madhara kutokana na maji yanayo tiririka kutoka mgodini kudaiwa kuwa na sumu.
Picha hapo chini zinaonesha baadhi ya wananchi walio athiriwa na maji hayo.
 
 

 
Pia jamii isisahau hata kidogo kile kilichotokea mwaka 2009, ambapo kemicali-sumu aina ya CYANIDE ilivuja na kuchanganyikana na maji yamto THIGITE, mto unaotumiwa na wanakijiji wa Nyamongo kama chanzo kikuu cha maji ya matumizi ya kila siku. Kutokana na tukio hilo, inakadiriwa watu wapatao Arobaini (40) walipoteza maisha, mamia wakiachwa na ulemavu wa kudumu na mifugo zaidi ya Mia Tano (500) ilikufa kutokana na kutumia maji yaliyochanganyikana na kemikali hiyo yenye sumu

 
 

 

Monday, February 1, 2016

IRINGA WAPONGEZA MRADI, WAPANDA MITI 45,000 KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA


Wakazi wa kijiji cha Kiwere wilaya ya Iringa vijijini wametoa shukrani zao za dhati kwa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) na kwa Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa kuendesha mradi wa ‘Ushiriki wa wananchi katika Kusimamia Maliasili’.

Akiongea wakati wa tathimini ya mafunzo ya mradi, kiongozi wa kikundi cha kuhifadhi mazingira (Kiwere Hifadhi Mazingira), Hamza Chang’a alisema, kabla ya mradi alikuwa na uelewa wa kawaida kuwa ukataji miti hauruhusiwi kwa kuwa unaharibu mazingira, hakuelewa kuwa wananchi wanao wajibu wa kulinda mazingira na maliasili kwa maendeleo endelevu na kuwa jambo hilo limeelezwa katika katiba ya nchi.

“Nilipoona watu wakikata miti, niliona ni jambo la kawaida, sikufahamu athari ya muda mrefu itokanayo na vitendo hivyo, namna vianavyo athiri ubora wa maisha ya sasa na vizazi vijavyo. Nilidhani ni wajibu wa kamati ya maliasili ya kijiji na viongozi wa kijiji kulinda maliasili, aliongeza.

Alisema mafunzo yamemwongeza ufahamu, yamebadilisha mtazamo kuhusu usimamizi wa maliasili, na ameanza kutumia ujuzi wake kwa vitendo kama mwananchi muwajibikaji.

Aliendelea kusema kuwa amepata dhana kamili ya ushiriki katika michakato wa maendeleo hivyo atajitolea kushawishi, kufanya kampeni na kufuatilia utekelezaji wa huduma za jamii.

Baada ya mafunzo, Chang’a na wenzake 16 waliunda kikundi cha kuhifadhi mazingira na katika kipindi cha miezi minne wamepanda zaidi ya miti 45,000 aina ya Mijoholo na Mikaratusi. Miti hiyo itapandwa katika eneo la msitu wa Msuni lilio haribiwa kutokana na ukataji miti hovyo na uchomaji mkaa.

Kwa upande wake Devotha Mihayo alisema, amejifunza kuwa uharibifu wa mazingira una athari kubwa kwa jamii hususan kwa wanawake. Unaathiri vyanzo vya maji, unasababisha ukame na njaa katika jamii. ‘Iwapo vyanzo vya maji vita haribiwa tutalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji, ambapo utatupotezea muda na kuweka maisha na afya zetu hatarini’ alisisitiza.

Alisema kuwa katika jamii yake hawaja wahi kushuhudia ukame kwa kuwa mvua inanyesha kwa wakati, lakini mafunzo yame watahadharisha kuhusu ukataji miti ambao unaweza kusababisha mabadiliko ya hali ya hewa hivyo kuleta mazalia ya mbu na kusababisha ugonjwa wa malaria. “Kila mmoja katika jamii yetu anahamasishwa kushiriki katika utunzaji wa mazingira wakati huo huo tukitunza afya zetu, zaidi ya hapo tuna hamasisha watoto kutoa taarifa za shughuli za uharibifu wa mazingira ilituchukue hatua za kuzuia haraka iwezekanavyo, alisema.

Naye Mashaka Kalinga Katibu Mtendaji wa asasi ya kiraia ya MJUMIKK, alithibitisha kuwa kijiji kimefanya jitihada nyingi za kuanzaisha uvunaji endelevu ili kuongeza mapato na kuhakikisha kuwa mapato yanayopatikana yananufaisha jamii. Zaidi ya hayo, serikali ya kijiji imezuia uchomaji mkaa, uvunaji miti usio endelevu, wameimarisha ulinzi na wanahamasisha wananchi kushiriki jitihada hizo.

Jumla ya wananchi 75 kutoka katika kamati za vijiji zikiwemo, kamati ya ardhi, kamati za mazingira na maliasili, baraza la ardhi, kamati ya maliasili ya wilaya na wawakilishi wa wananchi kutoka makundi mbalimbali, walihudhuria mafunzo ya Mradi wa Ushiriki wa wananchi katika Kusimamia Maliasili.

Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira kinatekeleza mradi wa miaka minne unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani, mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Kusimamia Maliasili, katika wilaya za Iringa na Mufindi, mkoani Iringa. Mradi ulianza mwaka 2014 na unatarajiwa kumalizika mwaka 2017.

 
Kiongozi wa ‘Kiwere Hifadhi Mazingira’, Hamza Chang’a na mwanakikundi Bruno Mpagama wakionesha sehemu ya miti 45,000, waliyo otesha katika bustani kijijini Kiwere
 
Katika picha ya pamoja ni baadhi ya washiriki wa mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Kusimamia Maliasili, Kijijini Kiwere