Saturday, May 21, 2016

KIKUNDI CHA UFUGAJI NYUKI CHA KIJIJI CHA IHEFU WILAYA YA MUFINDI WAHITIMU MAFUNZO

Timu ya watu 22 wa kikundi cha ufugaji nyuki katika kijiji cha Ihefu wilayani Mufindi, wahitimu mafunzo ya siku tatu ya ufugaji nyuki.
Mafunzo hayo ambayo hutolewa na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo(LEAT) yanalenga kuwezesha wananchi kuanzisha shughuli mbadala za kuongezea kipato katika vijiji 32 vinavyotekeleza mradi wa 'Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili' ...unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). 

 Katika awamu ya kwanza ya mafunzo ya ufugaji nyuki wanakikundi walijifunza umuhimu wa asali kwa matumizi ya kila siku, aina za nyuki, ufugaji bora, jinsi ya kutundika mizinga na uvunaji bora.

Awamu ya pili ya mafunzo itahusu usindikaji na jinsi ya kutafuta masoko ndani na nje ya nchi.
Baada ya kuhitimu mafunzo kila mshiriki alipewa vitendea kazi ambavyo ni mzinga wa nyuki, nta, patasi na vifaa vya kujikinga na nyuki- kofia, wavu wa kuzuia uso, glavu, suti na viatu maalum.
Mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili unatekelezwa katika vijiji 32 vya wilaya za Iringa na Mufindi katika mkoa wa Iringa.

 Wilaya hizo zilichaguliwa kwasababu zina maeneo ya usimamizi wa wanyamapori, rasilimali za wanyamapori, misitu na maeneo ya hifadhi. Lengo kuu la mradi ni kuhakikisha kuwa wananchi wanashiriki kikamilifu katika usimamizi wa maliasili.
Pia kutetea usimamizi bora wa maliasili ilikupunguza umasikini na kuhakikisha uhifadhi endelevu wa uhainuai, kuiwezesha jamii kuwa na utamaduni wa ushiriki katika masuala yanayohusu maliasili, kuzijengea uwezo jamii za wenyeji uwezo wa katika kuziwajibisha na kuzisimamia taasisi za serikali zenye majukumu ya kuhifadhi na kusimamia maliasili.
Sehemu ya wanakikundi cha ufugaji nyuki wakiwa darasani


Baadhi ya wanakikundi cha ufugaji nyuki wakiwa katika mavazi ya kujikinga na nyuki

Wanakikundi cha ufugaji nyuki wakifuatilia mafunzo
 
 

Friday, May 13, 2016

MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MALIASILI KATIKA KIJIJI CHA KINYIKA-WILAYA YA IRINGA

Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa kushirikiana na Asasi ya MBOMIPA ambao ni watekelezaji wenza katika mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, wamehitimisha mafunzo ya siku saba katika kijiji cha Kinyika, wilaya ya Iringa.

 Kijiji cha kinyika ni moja ya vijiji vilivyopo katika eneo la Usimamizi wa Wanyamapori linalosimamiwa na Asasi ya MBOMIPA, hivyo mafunzo hayo ni muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wa maeneo hayo; wanafahamu haki yao ya kikatiba katika kusimamia rasilimali misitu na wanyamapori kwa maendeleo endelevu ya kizazi cha sasa na kijacho.

 Hapa nchini na maeneo mengine duniani, kumezuka wimbi la watu wachache kuvuna rasilimali misitu na wanayamapori kwa manufaa binfsi ambayo si rafiki kiuchumi na kimazingira. Tumeshuhudia wanyapori wakiuawa kwa kasi sana na hasa tembo, simba na chui.

Pia katika sekta ya misitu tumeshuhudia uvunaji haramu na usio endelevu unao hatarisha hatma ya kizazi hiki.
Mafunzo hayo yalihusu mambo muhimu katika usimamizi dumivu wa misitu na wanyamapori, kwa kuangalia sera na sheria zinasema nini katika kusimamia rasilimali hizo. Pia, washiriki waliangalia miongozo, kanuni na adhabu, ambazo zitawasaidia katika kutengeneza sheria ndogondogo za vijiji za usimamizi wa maliasili.

Mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili umefadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). Mradi unatekelezwa katika vijiji 32 vya wilaya za Iringa na Mufindi, mkoani Iringa.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo wakijibu maswali ya awali kabla ya mafunzo, ilikupima wanaelewa kiasigani dhana ya Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa maliasili
 
 
 
Washiriki wa mafunzo katika kazi za vikundi
 
Afisa Ugani wa LEAT, Hana Lupembe (aliye vaa gauni jekundu) katika piacha ya pamoja na Washiriki wa mafunzo

WANANCHI WA VIJIJI VYA IFWAGI NA LUDILO WANOLEWA

Wananchi wa vijiji vya Ifwagi na Ludilo katika Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa wahudhuria mafunzo ya siku saba yaliyotolewa na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo' (LEAT) kwa kushirikiana na Asasi ya Kiraia ya ASH-TECH ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa 'Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili', unaofadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Kwa mujibu wa Afisa Ugani wa LEAT kwa wilaya ya Mufindi, Franklyn Masikia, takribani wananchi 120 walihudhuria mafunzo hayo, ambayo yalihusu Usimamizi wa Maliasili na Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wananchi kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa rasiliami misitu na wanyamapori, ilikuzinusuru na hatari ya kutoweka kutokana na kukithiri kwa uvunaji usio endelevu.

 Pia kupitia mafunzo ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Jamii, wananchi watakuwa na uwezo wa kuwa wajibisha viongozi wao kwa kudai uwazi katika kupanga matumizi ya maliasili, sambamba na kuhoji mapato na matumizi yatokanayo na rasilimali zinazopatikana katika vijiji vyao.
Mafunzo hayo yalianza mwanzoni mwa mwezi Mei, katika nyakati tofauti, ambapo kila kijiji kilikuwa na washiriki 60.

Katika mafunzo hayo, wananchi walipata fursa ya kuzifahamu sera, sheria na miongozo katika usimamizi dumivu wa maliasili. Pia, Washiriki waliweza kuona wajibu na umuhimu wa wadau mbalimbali katika sekta ya maliasili, ikiwemo taasisi zinazo simamia, mashirika ya kijamii ya kitaifa na kimataifa, wizara, pamioja na wajibu wa wananchi katika usimamizi wa maliasili.

  Mradi huu unatekelezwa katika vijiji 32 vya wilaya za Iringa vijijini na Mufindi, mkoani Iringa. Takriban wananchi 6500 watafikiwa na mradi huu.

Sehemu ya Washiriki wa mafunzo katika kijiji cha Ludilo wakimsikiliza Mwezeshaji kutoka Asasi ya ASH-TECH, Thomas Mtelega
Katika picha ya pamoja na Washiriki wa mafunzo kijiji cha Ifwagi

Wednesday, May 11, 2016

WANANCHI WA KIJIJI CHA MWITIKILWA WAJIPANGA UFUGAJI NYUKI


 Kikundi cha wafugaji nyuki cha kijiji cha Mwitikilwa cha wilaya ya Mufindi chajipanga kuzalisha asali kwa wingi ilikukidhi mahitaji katika jamii.
Kikundi hicho cha watu 22 kilihudhuria mafunzo ya siku tatu mahususi kwa ufugaji bora na wenye tija. Baada ya mafunzo kikundi kilipatiwa vitendea kazi, vikiwemo suti, glavu, kofia, wavu wa kujikinga uso, viatu, patasi na nta.

 Mafunzo ya ufugaji nyuki ni sehemeu ya utekelezaji wa mradi wa 'Ushiriki wa Wananachi katika Usimamizi wa Maliasili' mradi unaotekelezwa na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa ufadhili wa watu wa Marekani, kupitia shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). Mradi unatekelezwa katika vijiji 32 vya wilaya mbili za mkoa wa Iringa, wilaya ya Mufindi na Iringa.

 Lengo la mafunzo ya ufugaji nyuki ni kusaidia jamii zinazoishi karibu na rasilimali misitu na wanyamapori, kuinua uchumi wao bila ya kutegemea zaidi katika rasilimali zinazo wazunguka. Rasilimali ambazo ni chache na zinazo hitaji kutunzwa vizuri kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.

Mafunzo haya yalitolewa na Afisa Nyuki wa wilaya ya Mufindi, Hamis Hassan, na Thomas Mtelega wa Asasi ya ASH-TECH ambao ni washiriki wa utelekezaji wa mradi.

Wanakikundi cha ufugaji nyuki wakifuatilia mafunzo kutoka kwa Afisa Nyuki wa Wilaya ya Mufindi bwana Hamis Hassan (Hayupo pichani)


Baadhi ya wanakikundi cha ufugaji nyuki wakiwa na Afisa Nyuki wa Wilaya ya Mufindi bwana Hamis Hassan (wa kwanza kushoto mstari wa mbele-mwenye koti la bluu bahari bila kofia)

 

MAANDALIZI YA UFUGAJI NYUKI YAKAMALIKA KATIKA KIJIJI CHA LUDILO-WILAYA YA MUFINDI


 Tarehe 8 Mei 2016, Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) iligawa mizinga 22 kwa kikundi cha wafugaji nyuki 22 wa kijiji cha Ludilo, wilayani Mufindi katika mkoa wa Iringa.
Wanakikundi pia walipatiwa nyenzo muhimu iliwaweze kutekeleza kazi hiyo kwa ufanisi. Nyenzo hizo ni pamoja na suti maalum, kofia, wavu wa kujikinga usoni, glavu, viatu, patasi na nta.

Kabla ya kugawiwa mizinga kikundi kilipatiwa mafunzo ya siku tatu ya ufugaji nyuki ambapo walijifunza namna bora ya ufugaji nyuki, aina za nyuki na umuhimu wa asali kwa matumizi ya kila siku. Pia, kikundi kitapatiwa mafunzo ya namna ya kufungasha asali na utafutaji masoko.

 Kutokana na umihumu wa asali kwa matumizi ya kila siku, kumekuwa na mwamko mkubwa wa watu kutumia asali, hali hiyo inatoa fursa za ajira kwa wakazi wa maeneo yanayofuga nyuki.

Mradi wa ufugaji nyuki ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, unaotekelezwa na Timu wa Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

Moja ya lengo la mradi ni kuhakikisha kuwa Wananchi wanaoishi katika maeneo yenye rasilimali misitu na wanyamapori wanashiriki kikamilifu kuhifadhi na kulinda maliasili hizo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Ilikufikia lengo hilo, mradi wa ufugaji nyuki ni moja ya njia zitakazo wasaidia wananchi kupata vipato bila ya kutegemea rasilimali misitu, na wanyamapori; ilikuwa na mpango dumivu wa rasilimali hizo.
Afisa akisaidia kumvalisha glavu mmoja wa wanakikundi cha kufuga nyuki

Kikundi cha ufugaji nyuki katika mavazi rasmi ya kujikinga na nyuki mbele ya wananchi wa kijiji cha Ludilo

 

TUNASONGA MBELE-MAFUNZO YA UFUGAJI NYUKI IFWAGI-Wilaya ya Mufindi-Iringa


 MAFUNZO YA UFUGAJI NYUKI IFWAGI-Wilaya ya Mufindi, Iringa
Kikundi cha ufugaji nyuki cha watu 22 cha kijiji cha Ifwagi, wilaya ya Mufundi chapatiwa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa siku tatu, pamoja na mizinga 22 ya kufugia, na vifaa vya kujikinga na nyuki ambavyo ni kofia, wavu wa kujikinga usoni, glavu, na viatu maalumu. Pia walipatiwa  patasi na nta.

 Baada ya mafunzo wanakikundi cha ufugaji nyuki, Afisa Nyuki wa wilaya ya Mufindi, mwakilishi wa Asasi ya ASH-TECH pamoja na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazinigira kwa vitendo(LEAT), walitembelea msitu wa asili wa Kidege ili kuainisha eneo litakalo tundikwa mizinga ya nyuki.

 Mafunzo ya ufugaji nyuki yanawapatia wakazi wa kijiji cha Ifwagi chanzo mbadala cha mapato, ilikupunguza utegemezi wa mapato yatokanayo na rasilimali za msitu wa asili wa kidege. Msitu wa asili wa Kidege unategemewa na vijiji vitatu ambavyo ni Ifwagi, Mwitikilwa na Ludilo.


Mradi wa ufugaji nyuki utasaidia kupunguza utegemezi wa mapato unaotokana na rasilimali misitu na wanyamapori katika vijiji ambavyo vinatekeleza mradi wa 'Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili', unaotekelezwa na LEAT katika vijiji 32 vya wilaya za Iringa na Mufindi, mkoani Iringa.

 
 Mradi wa Ushiriki wa Wananachi katika Usimamizi wa Maliasili unafadhiliwa na Watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID), ulianza Novemba 2014 na unatarajiwa kukamilika Novemba 2017.

Baadhi ya Wanakikundi wakiwaonesha wenzao namna ya kutundika mzinga wa nyuki baada ya mafunzo. Aliyevaa koti jeusi ni Afisa Nyuki wa Wilaya ya Mufindi bwana Hamis Hassan.
 
Wanakikundi wakifuatilia mafunzo
Wanakikundi wakiwa na Afisa Nyuki wa Wilaya ya Mufindi, Hamis Hassan (wa pili kushoto) Boksi jeupe linalo ning'inia kwenye mti ni moja ya mizinga iliyogawiwa na LEAT kwa kikundi hicho.
 
.

 

Saturday, May 7, 2016

VIKUNDI VYA UFUGAJI NYUKI VYAPATIWA VITENDEA KAZI

Vikundi vya ufugaji nyuki katika vijiji vya Malinzanga, Kiwere, Mfyome, Kitapilimwa, Itagutwa, Kitisi na Idodi. Kila kijiji kina kikundi kimoja chenye watu 22. Baada ya kupatiwa mafunzo ya ufugaji nyuki kila mwanakikundi alipatiwa mzinga wa kufugia nyuki, na awamu ya pili walipatiwa vifaa vya ufugaji nyuki ikiwa ni pamoja na kofia, nyavu, glavu, suti na viatu maalumu vya kujikinga na nyuki. Zifuatazo ni picha za ugawaji wa vitendea kazi hivyo.
Afisa Vifaa bwana Mremi akiteremsha vifaa vya ufugaji nyuki tayari kwa kuwagawia wanakikundi cha ufugaji nyuki wa kijiji cha Idodi, wilayani Iringa

 
Wa pili kushoto afisa Ugani, Hana Lupembe akiwa pamoja na wanakikundi cha ufugaji nyuki wa kijiji cha Idodi. Mmoja wa wanakikundi akiwa amevalia mavazi rasmi ya ufugaji nyuki
 
Afisa Vifaa bwana Mremi akisaidia kumvalisha mavazi ya kujikinga na nyuki, mmoja wa wanakikundi cha ufugaji nyuki wa kijiji cha Kitisi

Afisa Ugani Hana Lupembe akimkabidhi Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kitisi, vifaa vya kujikinga na nyuki kwaajili ya wanakikundi wa ufugaji nyuki. Wanao shuhudia ni baadhi ya wanakikundi cha ufugaju nyuki

Mwenyekiti wa Asasi ya MJUMIKK ambao ni wadau wa utekelezaji wa maradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, Mashaka Kilanga, akimuelekeza mmoja wa wanakikundi cha ufugaji nyuki jinsi ya kuvaa mavazi ya kujikinga na nyuki katika kijiji cha Itagutwa, wilaya ya Iringa
 
KIJIJI CHA KITAPILIMWA-TENDA KAMA MWENYE MALI!
Afisa Ugani Hana Lupembe akiwa anatafuta mtandao wa simu kwaajili ya kuwasiliana na Makao Makuu Dar es Salaam. Ilimlazimu apande juu ya mti kutafuta mawasilino.
 

Kutoka kulia: Afisa Ugani Hana Lupembe na bwana Komba (mwenye nguo nyeusi) wakiwa na baadhi ya wanakikundi cha ufugaji nyuki kijijini Kitapilimwa
 
 
(Wa tatu kushoto)Mwenyekiti bwana Kilanga na (wa pili kushoto)Mratibu bwana Komba wa Asasi ya MJUMIKK, wakipata maelezo kutoka kwa kikundi cha ufugaji nyuki, walipo tembelea enao la kufugia nyuki kijijini Kitapilimwa

Afisa Ugani, Hana Lupembe akisoma orodha ya vifaa vya kujikinga na nyuki alivyokabidhi kwa kikundi cha ufugaji nyuki- Mfyome


Mwanakikundi cha ufugaji nyuki akiwa katika mavazi ya kujikinga na nyuki katika eneo la kufugia nyuki- Mfyome


Afisa Ugani, Hana Lupembe akikagua mizinga iliyotundikwa katika eneo la kufugia nyuki katika kijiji cah Kiwere, wilaya ya Iringa
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kiwere (mwenye koti jeusi) alipewa heshima na LEAT ya kugawa vifaa vya kujikinga na nyuki kwa wanakikundi cha ufugaji nyuki-Kiwere

Katika picha ya pamoja: Kutoka kulia waliokaa: Afisa Mtendaji wa kijiji cha Kiwere, Mratibu wa Asasi ya MJUMIKK, Mwenyekiti wa Asasi ya MJUMIKK na mwanakikundi cha ufugaji nyuki.
Waliosimama kutoka kulia: Afisa Ugani Hana Lupembe akiwa na baadhi ya wanakikundi cha ufugaji nyuki, baada ya kugawiwa mavazi ya kujikinga na nyuki.


Mwanakikundi cha ufugaji nyuki wa kijiji cha Malinzanga akivaa mavazi ya kujikinga na nyuki, mara baada ya kugawiwa na LEAT.
Kuelekea eneo la ufugaji nyuki- Iliwalazimu kuacha gari mbali kigodo- Afisa Vifaa bwana Mremi akivuka mto kuelekea eneo la kufugia nyuki-Malinzanga
Eneo la kufugia nyuki Malinzanga-Wanakikundiwakionesha mizinga waliyotundika