Monday, June 12, 2017

MAZINGIRA NI LAZIMA YAHIFADHIWE.




Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Amina Masenza kwa mara nyingine amesisitiza kuwa Mazingira katika Mkoa huo ni lazima yahifadhiwe na kulindwa kwani itasababisha baadhi ya wananchi kuathiriwa kwa namna mbalimbali endapo wataendelea kufanya shughuli zinazoathiri Mazingira.


Mkuu wa Mkoa ametoa Msimamo huo katika kilele cha wiki ya Mazingira ambayo Kimkoa imeadhimishwa katika kijiji cha Mangalali wilaya ya Iringa.


Katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala Msaidizi idara ya Mipango, Bw. Nuhu Mwasumilwe, Mkuu wa Mkoa ametoa changamoto kwa wataalam kufikiri tofauti ili kuja na njia mbadala itakayosaidia kupunguza shughuli zinazosababisha uharibifu wa Mazingira. Na hii ni kutokana na ukweli kuwa, kwa sasa kila mmoja ameshaguswa na athari zinazosababishwa na uharibifu wa Mazingira.



Afisa Maliasi wa Mkoa wa Iringa amesema baadhi ya shughuli zinazofanywa ili kusaidia uhifadhi wa Mazingira ni pamoja ufugaji wa nyuki ambapo mpaka sasa Mkoa unakadiriwa kuwa na mizinga elfu thelathini (30,000) ya watu na vikundi mbalimbali ambapo Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira (LEAT) kupitia mradi wake wa Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani USAID, ni moja ya wadau waliochangia mizinga hiyo kwa kutoa mizinga 704 kwa vijiji 32 Mkoani Iringa.

 Kikundi cha sanaa Mashujaa kutoka Mfyome wilayani Iringa, wakihamasisha wananchi kutunza mazingira katika kilele cha siku ya mazingira duniani, ambayo kimkoa ilihadhimishwa kijiji cha Mangalali, mkoani Iringa.

 Mgeni Rasmi, Katibu Tawala Msaidizi idara ya Mipango, Bw. Nuhu Mwasumilwe akipanda mti ikiwa kama kumbukumbu ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani katika kijiji cha Mangalali, wilayani Iringa.

 Kikundi cha sanaa Mashujaa kutoka kijiji cha Mfyome wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuamaliza tukio la kupanda mti wa kumbukumbu katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, kijiji cha Mangalali, Mkoani Iringa.

Afisa Habari na Mawasiliano kutoka LEAT akitoa salamu katika maadhimisho ya kilele cha siku ya mazingira duniani, ambayo kimkoa yalifanyika kijiji cha Malangali, wilayani Iringa, Mkoani Iringa.

Saturday, June 3, 2017

PROF. ANNA TIBAIJUKA ATAMKA KUWA GHARAMA YA SERIKALI KUIPUUZA LEAT IMEONEKANA




Mkutano wa Saba wa Bunge umeendelea Dodoma. Kazi kubwa ikiwa ni mapendekezo ya wabunge katika bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ambapo miongoni mwa waliopata nafasi ya kuchangia ni Mbunge wa Muleba Kusini Professor Anna Tibaijuka.

"Mhe Spika kuna Taasisi ya Lawyers' Environmental Action Team (LEAT) ina vijana wamekaa  vizuri sana. Sasa wamekuwa wakipuuzwa wakati wote na gharama ya kupuuzwa mnaiona". Alisema Prof. Anna Tibaijuka.

"Tuweke utamaduni wa kuwaheshimu na kuwasikiliza wataalam wetu. Tukiendelea kuwaita wanaharakati huku tukiwabeza na kuwapuuza, hatutatoka hapa tulipo". Aliongezea Prof. Tibaijuka


Tafadhali fungua video hiyo hapo juu kupata taarifa kwa kirefu.

Thursday, June 1, 2017

SEMA KWELI - Tulifikaje na Tunatokaje kisheria




Dr. Rugemeleza Nshala, Mkurugenzi Mtendaji wa Timu ya

Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT),

amezungumzia suala la Makinikia katika kipindi cha "Sema Kweli"

kilichorushwa tarehe 31.05.2017, saa nne (4) usiku kupitia 

Chanel 10.


Hii ni kutokana na Ripoti ya kamati maalumu ya Rais wa Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania juu ya uchunguzi wa kiwango cha

madini.


Dr.Nshala akiwa kama Mwanasheria aliyebobea kwenye masuala

ya mazingira, analizungumzia suala la Madini kwa upana wake. Na 
kuelezea tumefikaje hapa tulipo na tutatokaje kisheria.

Lengo ni kuisaidia nchi, serikali yetu na pengine kumshauri Mhe. 

Rais namna ya kutoka hapa tulipo.



Tafadhali fungua video hapo juu kufuatilia kipindi hiko

Thursday, May 25, 2017

Tamko la LEAT juu ya Ripoti ya Kamati Maalum ya Rais kuhusu Mchanganyiko wa Madini katika Makontena.

Timu ya Wanaseheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo 
(LEAT) Imetoa tamko juu ya Ripoti ya Kamati Maalumu ya Rais juu ya Mchanganyiko wa Madini (Makinikia) katika Makontena yaliyozuiliwa bandarini.

Kwa kifupi LEAT haishangazwi na kile kilichobainika kwani 
ni kile ilichokuwa inakisema miaka yote tokea mwaka 2001. 
LEAT inataka mabadiliko makubwa katika sekta za mafuta, gesi na madini kwani sheria zinazoziongoza zinaruhusu kuporwa kwa rasilimali hizi muhimu za nchi.


Fungua link hii kusoma Tamko hilo.


Monday, May 22, 2017

International Day for biological biodiversity: celebrate by protecting biodiversity, not promoting tourism.


21 May, 2017


Tourists waiting to take photographs  of orangutans during feeding 
time at Sepilok Orang Utan Rehabilitation Centre,  
Sabah, 
Malaysia.© Center for Intern
ational Forestry 
Research


22 May 2017 is International day for biodiversity and this year’s theme is tourism. The UN Convention on biodiversity (CBD) is using this opportunity to promote the value of tourism in significantly reducing threats to, and maintaining or increasing key wildlife populations and biodiversity through tourism revenue. It does mention the need to reduce the negative impacts of tourism but, whereas it sings the supposed values of tourism, it merely whispers the negative impacts.

Positive examples of tourism do exist, such as Community Based Tourism projects, which protect territories, livelihoods and cultures. Friends of the Earth has worked with several such initiatives around the world, such as community based eco-curtural tourism in Timor Leste.  Self-governance is essential, as are revenues that go directly to the local community and respect for their traditional ways of generating income. Unfortunately many initiatives don’t survive without the help of NGOs. 

Sadly few sustainable tourism projects are actually viable. 
For example many “ecotourism” initiatives, whilst better for the environment, fail local communities by denying them revenue generation and self-determination. On a global scale, positive tourism is minimal. Yet the few examples that exist are being used to suggest that the entire tourism sector could become sustainable.

The biggest culprit of unsustainable and economically unjust tourism remains mainstream tourism. Indigenous peoples are often evicted from their land to make way for tourist resorts. Human rights abuses are rife, with some cases ending in death for people protecting their land. Hotels are often built on valuable ecosystems, destroying them in the process. Proposals such as the El Salvadoran Government’s tourism project in 2013 which threatened both coastal mangrove forests and local communities often fall foul of more than one injustice. 

Young boy swimming in mangroves in La Tirana, El Salvador ©Friends of the Earth International / Jason Taylor

Indigenous people are often banned from their own territories as sacred sites are privatized, so tourists can enjoy them undisturbed. The profit from tourist resorts remains in the hands of transnational corporations. Furthermore local people are often exploited as workers in these resorts and hotels. A person’s water usage in hotels is significantly higher than at home.  In some cases tourists use 16 times as much water as locals, causing conflict and disease.

Food waste is a huge issue. Even small resorts waste up to 150 tons of food a year, and a staggering 36% of all food purchased ends up in the bin. Cruise liners dump up to 3.8billion litres of sewage in the oceans polluting ecosystems. These are just a few of the issues generated by mainstream tourism.

Sustainable tourism initiatives usually mean a mere change in the levels of waste and energy consumption rather than a change of business model. Initiatives are purely voluntary, a practise which has proved disastrous in other economic sectors. 

It seems unlikely that tourism can become a green industry. 5% of global emissions are linked to tourism, purely for the benefit of richer middle and higher classes. The aviation industry alone plans 700% growth by 2050. It plans to offset its increased emissions through REDD programs. REDD is a false solution and desperately unsustainable.  

Tourism comprises 10% of the global GDP with a projected annual growth of 3-5%. It does not need the promotion for economic development the UN is giving it on this day of International biodiversity.

What tourism needs is policies that respect the rights of local communities and indigenous peoples,
including their right to self-determination, the visitors they receive, a fair share of the revenue, and protection for their ecosystems. Official studies on the negative impacts of corporate tourism and tough measures to prohibit the worst practices are desperately needed. Please help us celebrate International biodiversity day by calling for a change in the tourism business model.

Tuesday, April 11, 2017

Timu ya SAM ya Wilaya ya Iringa yatoa mrejesho na tathimini ya usimamizi wa maliasili kwa Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa





Mkuu wa wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesela ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa, kutoa maelezo ama kumwajibisha Mtumishi anayekwamisha shughuli za uhifadhi wa Mazingira katika wilaya hiyo.


Kutokana ripoti iliyowasilishwa mwaka jana na Timu ya SAM ya wilaya ya Iringa inayowezeshwa na LEAT kupitia msaada wa watu wa Marekani USAID, iliweza kuibua changamoto mbalimbali za usimamizi wa maliasili na kutoa mapendekezo kwa halmashauri ya wilaya ya Iringa kujaribu kutatua changamoto hizo za kimazingira. Bw. Kasesela alisema walikubaliana mambo mbalimbali yatatekelezwa lakini mpaka hivi, asilimia 80 ya mambo hayo hayajatekelezwa kutokana na baadhi ya watumishi
kutotimiza wajibu wao.


Mkutano huo wa mrejesho wa shughuli za usimamizi wa maliasili uliofanya na Timu ya SAM ya wilaya ya Iriniga kwa kushirikiana na LEAT, ulihudhuriwa na wataalamu na Maafisa wa wilaya ya Iringa, Mkurugenzi wa wilaya na wafanyakazi kutoka LEAT. 

Afisa Mwandamizi wa mradi wa CEGO Bw. Remmy Lema alisema, Pamoja na elimu na kuwasaidia kuboresha sheria za vijiji, katika mradi wa ushiriki wa Wananchi katika usimamizi wa maliasili zao (CEGO), unaofadhiliwa na Shirika la misaada la Marekani USAID, Timu ya watetezi wa Mazingira kwa vitendo LEAT pia imetoa mizinga ya nyuki kwa vijiji kama njia mbadala ya wananchi hao kujikimu kimaisha na tayari
wameshatoa mizinga ya nyuki 704.

Saturday, April 8, 2017

TIMU YA SAM YA WILAYA YA MUFINDI YAFANYA ZIARA YA KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA USIMAMIZI WA MALIASILI KATIKA VIJIJI VYA MRADI.


Wajumbe wa Timu ya SAM ya Wilaya ya Mufindi wakifanya mahojiano na uongozi wa kijiji cha Igombavanu juu ya usimamizi wa maliasili za kijiji hicho


Wajumbe wa Timu ya SAM ya Wilaya ya Mufindi wakifanya mahojiano na uongozi wa kijiji cha Mapogoro  juu ya usimamizi wa maliasili za kijiji hicho
Mjumbe akibainisha changamoto za usimamizi wa maliasi katika kijiji cha Ikangamwani
Mwenyekiti wa Timu ya SAM wilaya ya Mufindi Bw. Clemence Mwapelwa akiitambulisha Timu ya Ufuatiliaji wa Ufuatiliaji jamii kwa uongozi wa kijiji cha Ikangamwani

Wajumbe wa Timu ya SAM wakifanya tathmini ya pamoja juu ya mafanikio na changamoto za usimamizi wa maliasili kutokana na ziara zilizofanyika katika vijiji vya Igombavanu, Idumlavanu, Ikangamwani na Mapogoro
Timu ya SAM ya Wilaya ya Mufindi yatembelea vijiji vya mradi vinne ambayo ni Igombavanu, Mapogoro, Idumlavanu na Ikangamwani,  ili kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za usimamizi wa maliasili kuanzia ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji.


Pia Timu hiyo ililenga kupima matokeo ya utekelezaji wa shughuli za mradi ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya jinsi halmashauri ya wilaya ilivyotekeleza mapendekezo ya Timu hiyo kama yalivyowasilishwa mwaka jana 2016.


Katika ziara hii Timu iliweza kukutana na baadhi ya wajumbe wa Kamati za maliasili za vijiji, Halmashauri za vijiji, Timu ndogo za SAM za vijiji, na Kamati za uchumi na fedha.


Lengo la kukutana na wajumbe hawa ni kuwahoji na kutoa mrejesho ambao utaisaidia Timu ya SAM ya wilaya kulinganisha kilichopo kwenye nyaraka na kinachotetendeka katika vijiji husika.


Taarifa itakayokusanywa na Timu hii itataja mambo ambayo yatahitaji muitikio kutoka kwa halmashauri za vijiji na halmashauri ya wilaya.


Ripoti itataja mafanikio na changamoto ambazo zimegunduliwa na timu ya SAM ya wilaya, ambazo zitawasilishwa mbele ya Mkurugenzi, Mkuu wa wilaya na Watendaji wakuu wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi.