Mkutano wa Saba wa Bunge
umeendelea Dodoma. Kazi kubwa ikiwa ni mapendekezo ya wabunge katika bajeti ya Wizara
ya Nishati na Madini ambapo miongoni mwa waliopata nafasi ya kuchangia ni
Mbunge wa Muleba Kusini Professor Anna Tibaijuka.
"Mhe Spika kuna Taasisi ya
Lawyers' Environmental Action Team (LEAT) ina vijana wamekaa vizuri sana. Sasa wamekuwa wakipuuzwa wakati
wote na gharama ya kupuuzwa mnaiona". Alisema Prof. Anna Tibaijuka.
"Tuweke utamaduni wa
kuwaheshimu na kuwasikiliza wataalam wetu. Tukiendelea kuwaita wanaharakati
huku tukiwabeza na kuwapuuza, hatutatoka hapa tulipo". Aliongezea Prof.
Tibaijuka
Tafadhali fungua video hiyo hapo
juu kupata taarifa kwa kirefu.
No comments:
Post a Comment