Mjumbe akibainisha changamoto za usimamizi wa maliasi katika kijiji cha Ikangamwani |
Mwenyekiti wa Timu ya SAM wilaya ya Mufindi Bw. Clemence Mwapelwa akiitambulisha Timu ya Ufuatiliaji wa Ufuatiliaji jamii kwa uongozi wa kijiji cha Ikangamwani |
Wajumbe wa Timu ya SAM wakifanya tathmini ya pamoja juu ya mafanikio na changamoto za usimamizi wa maliasili kutokana na ziara zilizofanyika katika vijiji vya Igombavanu, Idumlavanu, Ikangamwani na Mapogoro |
Timu
ya SAM ya Wilaya ya Mufindi yatembelea vijiji vya mradi vinne ambayo ni Igombavanu, Mapogoro, Idumlavanu na
Ikangamwani, ili kufanya tathmini ya
utekelezaji wa shughuli mbalimbali za usimamizi wa maliasili kuanzia ngazi ya Wilaya,
Kata na Vijiji.
Pia
Timu hiyo ililenga kupima matokeo ya utekelezaji wa shughuli za mradi ikiwa ni
pamoja na kufanya tathmini ya jinsi halmashauri ya wilaya ilivyotekeleza
mapendekezo ya Timu hiyo kama yalivyowasilishwa mwaka jana 2016.
Katika
ziara hii Timu iliweza kukutana na baadhi ya wajumbe wa Kamati za maliasili za
vijiji, Halmashauri za vijiji, Timu ndogo za SAM za vijiji, na Kamati za uchumi
na fedha.
Lengo
la kukutana na wajumbe hawa ni kuwahoji na kutoa mrejesho ambao utaisaidia Timu
ya SAM ya wilaya kulinganisha kilichopo kwenye nyaraka na kinachotetendeka
katika vijiji husika.
Taarifa
itakayokusanywa na Timu hii itataja mambo ambayo yatahitaji muitikio kutoka kwa
halmashauri za vijiji na halmashauri ya wilaya.
Ripoti
itataja mafanikio na changamoto ambazo zimegunduliwa na timu ya SAM ya wilaya,
ambazo zitawasilishwa mbele ya Mkurugenzi, Mkuu wa wilaya na Watendaji wakuu wa
Halmashauri ya wilaya ya Mufindi.
No comments:
Post a Comment