Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Bw. Stephen Mhapa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Bw. Joseph Chitika wakiongoza majadiliano katika mkutano wa baraza la wadiwani
Mwanasheria mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bi. Kissah Mbilla akifuatilia majadiliano ya baraza la madiwani wakati wa kupitisha sheria ndogo za vijiji
Baadhi ya wajumbe na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa baraza la madiwani wakifuatilia kwa makini kuidhinishwa kwa sheria ndogo za vijiji vya Mbweleli, Kinyali na Kinyika. |
Mkuu
wa Idara ya Ardhi na Maliasili wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Bw. Donald Mshani akihojiwa na waandishi wa habari baada ya baraza ya madiwani kuidhinisha sheria ndogo za vijiji husika
Mwanasheria
mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Bi. Kissah Mbilla akihojiwa na waandishi wa habari baada ya baraza ya madiwani kuidhinisha sheria ndogo za vijiji husika
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imeidhinisha kuanza kutumika
kwa sheria ndogo za usimamizi wa
maliasili ili kukabiliana na kasi ya uharibifu wa rasilimali za misitu na
wanyamapori katika vijiji vitatu miongoni mwa vijiji ambavyo LEAT inatekeleza
mradi wa ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa maliasili.
Sheria zilizoidhinishwa na halmashauri hiyo zimetungwa na
halmashauri za vijiji vya Mbweleli, Kinyika na Kinyali chini ya msaada wa Timu
ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT), lengo likiwa ni kudhibiti uharibifu wa mazingira
unaokuwa kwa kasi katika vijiji hivyo.
Mara baada ya baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya
Iringa kuidhinisha kuanza kutumika kwa sheria hizo katika kikao cha baraza la
madiwani kilichoketi tarehe 29/10/2016, Mwenyekiti wa halmashauri
hiyo Stephen Mhapa alisema sheria hizo
zitasaidia kuongeza kasi ya utunzaji wa mazingira na wanyamapori katika vijiji
husika.
Alisema Halmashauri za vijiji zina mamlaka kamili ya kutunga
sheria ndogo zinazohusu usimamizi wa maeneo yao na kwamba sheria hizo zisipingane
na sheria mama za nchi na Halmashauri husika.
“Kitendo cha halmashauri za vijiji kutunga sheria ndogo za
kusimamia na kudhibiti uharibifu wa maliasili katika maeneo yao kimenifurahisha
na kwamba kuanzia sasa misitu na wanyamapori waliokuwa katika hatari ya
kutoweka kutokana na ujangili na uchomaji moto watakuwa salama”alisema Mhapa:
“Hiyo ni kutokana na wananchi wa eneo husika wao wenyewe kwa
hiyari yao kujitungia sheria wanazoweza kuzisimamia, katika hili ninawashukuru Timu
ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa vitendo (LEAT) ambao wamewapatia elimu
na msaada wa kufikia hatua hiyo ya kutunga sheria ndogo watakazoweza
kuzisimamia wao wenyewe” alisema Mhapa.
Mwanasheria mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Kissah Mbilla alisema
jukumu la ofisi yake katika mchakato huo pamoja na kushirikiana na wanasheria
wa LEAT ilikuwa kuhakikisha sheria hizo ndogo hazipingani na sheria mama ambayo
ni ile ya Halmashauri na ya Nchi.
“Halmashauri ya kijiji inayo mamlaka ya kutunga sheria ndogo
na ofisi yetu inachofanya ni kuangalia kama taratibu zimefuatwa, adhabu
zinazotolewa katika sheria ndogo za kijiji hazizidi Tsh 50,000 na kwakuwa
wamepitisha na baraza la madiwani limeidhinisha sheria hizi, sasa ni sheria
kamili na zinaweza kuanza kutumika” alisema Mbilla.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili wa
Halmashauri hiyo Donald Mshani alisema kuidhinishwa kwa sheria hizo kutasaidia
idara yake kupambana na uharibifu wa mazingira ambao kwa sasa umekuwa ukishika
kasi.
Alisema hatua hiyo inaweza kuwa ya mafanikio kutokana na
sheria hizo tangu mchakato wa kutunga hadi kuidhinishwa na baraza la madiwani
umeshirikisha wananchi katika kufikia malengo hayo.
Afisa habari wa Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa
Vitendo (LEAT) alisema hatua ya baraza la madiwani kuidhinisha kutumika kwa
sheria hizo kumewafariji kwa kuwa jukumu lao la kuelimisha wananchi na
kuwahamasisha kutunga sheria hizo linakuwa limetimia.
Edina Tibaijuka alisema LEAT kupitia mradi wa Ushiriki wa
wananchi katika usimamizi wa maliasili unaofadhiliwa na shirika la Kimataifa la
watu wa Marekani (USAID) ilihamasisha halmashauri za vijiji vya Kinyali na
Kinyika kutunga sheria ndogo hizo kwani awali hawakuwa nazo kabisa na kwa
upande wa kijiji cha Mbweleli LEAT iliwawezesha Halmashauri ya kijiji hiko
kufanya marekebisho ya sheria yao baada ya kuipitia na kuona sheria waliyokuwa
wakiitumia awali ina mapungufu.
“Baada ya mikutano mikuu
ya vijiji hivyo kuridhia na kupitisha sheria hizo kuhusiana na maliasili
ziliwasilishwa katika ofisi ya mwanasheria wa wilaya, kisha zilijadiliwa na
kupitishwa na kamati husika za wilaya na kufikishwa katika baraza la madiwani
ambao waliridhia kuanza kutumika kwa sheria hizo na kunatoa fursa kwa serikali
za vijiji kuanza kuzitumia ili kudhibiti vitendo vya uharibifu wa mazingira” alisema.
Tibaijuka.
No comments:
Post a Comment