Thursday, April 6, 2017

SHERIA NDOGO

               



BARAZA LA MADIWANI LA WILAYA YA IRINGA LAIDHINISHA SHERIA NDOGO ZA USIMAMIZI WA MALIASILI  ZA KIJIJI CHA MBWELELI, KINYALI NA KINYIKA

Hatimae wananchi wa vijiji  vya Kinyika, Kinyali na
Mbweleli vilivyopo wilayani Iringa wamepitisha sheria ndogo zenye lengo la
kuhifadhi wanyama wa maeneo yao na utunzaji wa rasilimali za misitu zinazowazunguka.

Hatua hiyo inatokana na malalamiko ya muda mrefu ya
uharibifu wa mazingira na uuaji hovyo wa wanyama wanaokatisha kwenye vijiji
hivyo wakitokea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kuelekea Mikumi.

Sheria ndogo zilizizopitishwa na wananchi kwa msaada
wa Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo –LEAT inayofadhiliwa na USAID, na kuidhinishwa na
baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa huenda zikawa mwarobaini wa malalamiko ya madiwani
yanayosababishwa na kukithiri kwa uharibifu wa mazingira.


Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bi. Kissa Mbila amesema, "Sasa
kijiji kitakuwa na uwezo wa kusimamia sheria hizo kwa kuwaadhibu wanaoikiuka
sheria ndogo badala ya kutegemea Halmashauri na hivyo kuongeza ulinzi wa
raslimali zake".

Vijiji hivyo vinapakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na ni
miongoni mwa maeneo ambapo wanyama huvuka kwenda maeneo mengine.

LEAT inapongeza vijiji hivyo kutambua umuhimu wa uhifadhi wa maliasili zinazowazungukua na kufikia lengo la kuweza kupitisha sheria ndogo hizo. Pia inatambua mchango wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kwa kuidhinisha sheria ndogo hizo lakini pia mwandishi kutoka Televisheni ya Taifa TBC1 Bi Irene Mwakalinga kwa kuripoti taarifa hii.

No comments:

Post a Comment