Tuesday, April 11, 2017

Timu ya SAM ya Wilaya ya Iringa yatoa mrejesho na tathimini ya usimamizi wa maliasili kwa Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa





Mkuu wa wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesela ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa, kutoa maelezo ama kumwajibisha Mtumishi anayekwamisha shughuli za uhifadhi wa Mazingira katika wilaya hiyo.


Kutokana ripoti iliyowasilishwa mwaka jana na Timu ya SAM ya wilaya ya Iringa inayowezeshwa na LEAT kupitia msaada wa watu wa Marekani USAID, iliweza kuibua changamoto mbalimbali za usimamizi wa maliasili na kutoa mapendekezo kwa halmashauri ya wilaya ya Iringa kujaribu kutatua changamoto hizo za kimazingira. Bw. Kasesela alisema walikubaliana mambo mbalimbali yatatekelezwa lakini mpaka hivi, asilimia 80 ya mambo hayo hayajatekelezwa kutokana na baadhi ya watumishi
kutotimiza wajibu wao.


Mkutano huo wa mrejesho wa shughuli za usimamizi wa maliasili uliofanya na Timu ya SAM ya wilaya ya Iriniga kwa kushirikiana na LEAT, ulihudhuriwa na wataalamu na Maafisa wa wilaya ya Iringa, Mkurugenzi wa wilaya na wafanyakazi kutoka LEAT. 

Afisa Mwandamizi wa mradi wa CEGO Bw. Remmy Lema alisema, Pamoja na elimu na kuwasaidia kuboresha sheria za vijiji, katika mradi wa ushiriki wa Wananchi katika usimamizi wa maliasili zao (CEGO), unaofadhiliwa na Shirika la misaada la Marekani USAID, Timu ya watetezi wa Mazingira kwa vitendo LEAT pia imetoa mizinga ya nyuki kwa vijiji kama njia mbadala ya wananchi hao kujikimu kimaisha na tayari
wameshatoa mizinga ya nyuki 704.

Saturday, April 8, 2017

TIMU YA SAM YA WILAYA YA MUFINDI YAFANYA ZIARA YA KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA USIMAMIZI WA MALIASILI KATIKA VIJIJI VYA MRADI.


Wajumbe wa Timu ya SAM ya Wilaya ya Mufindi wakifanya mahojiano na uongozi wa kijiji cha Igombavanu juu ya usimamizi wa maliasili za kijiji hicho


Wajumbe wa Timu ya SAM ya Wilaya ya Mufindi wakifanya mahojiano na uongozi wa kijiji cha Mapogoro  juu ya usimamizi wa maliasili za kijiji hicho
Mjumbe akibainisha changamoto za usimamizi wa maliasi katika kijiji cha Ikangamwani
Mwenyekiti wa Timu ya SAM wilaya ya Mufindi Bw. Clemence Mwapelwa akiitambulisha Timu ya Ufuatiliaji wa Ufuatiliaji jamii kwa uongozi wa kijiji cha Ikangamwani

Wajumbe wa Timu ya SAM wakifanya tathmini ya pamoja juu ya mafanikio na changamoto za usimamizi wa maliasili kutokana na ziara zilizofanyika katika vijiji vya Igombavanu, Idumlavanu, Ikangamwani na Mapogoro
Timu ya SAM ya Wilaya ya Mufindi yatembelea vijiji vya mradi vinne ambayo ni Igombavanu, Mapogoro, Idumlavanu na Ikangamwani,  ili kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za usimamizi wa maliasili kuanzia ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji.


Pia Timu hiyo ililenga kupima matokeo ya utekelezaji wa shughuli za mradi ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya jinsi halmashauri ya wilaya ilivyotekeleza mapendekezo ya Timu hiyo kama yalivyowasilishwa mwaka jana 2016.


Katika ziara hii Timu iliweza kukutana na baadhi ya wajumbe wa Kamati za maliasili za vijiji, Halmashauri za vijiji, Timu ndogo za SAM za vijiji, na Kamati za uchumi na fedha.


Lengo la kukutana na wajumbe hawa ni kuwahoji na kutoa mrejesho ambao utaisaidia Timu ya SAM ya wilaya kulinganisha kilichopo kwenye nyaraka na kinachotetendeka katika vijiji husika.


Taarifa itakayokusanywa na Timu hii itataja mambo ambayo yatahitaji muitikio kutoka kwa halmashauri za vijiji na halmashauri ya wilaya.


Ripoti itataja mafanikio na changamoto ambazo zimegunduliwa na timu ya SAM ya wilaya, ambazo zitawasilishwa mbele ya Mkurugenzi, Mkuu wa wilaya na Watendaji wakuu wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi. 

Thursday, April 6, 2017

World Environmental Day





LEAT CELEBRATED THE WORLD ENVIRONMENTAL DAY 

LEAT celebrates the World  Environmental Day by participate in making sanitation in Mfyome village within Iringa district. 

Additional through Mfyome theater group which was established by LEAT, They performed and encouraged community members to do cleanliness In their surroundings, to avoid outbreak and spread of infectious diseases like cholera

LEAT YAHAMASISHA UPITISHWAJI WA SHERIA NDOGO

SHERIA NDOGO

               



BARAZA LA MADIWANI LA WILAYA YA IRINGA LAIDHINISHA SHERIA NDOGO ZA USIMAMIZI WA MALIASILI  ZA KIJIJI CHA MBWELELI, KINYALI NA KINYIKA

Hatimae wananchi wa vijiji  vya Kinyika, Kinyali na
Mbweleli vilivyopo wilayani Iringa wamepitisha sheria ndogo zenye lengo la
kuhifadhi wanyama wa maeneo yao na utunzaji wa rasilimali za misitu zinazowazunguka.

Hatua hiyo inatokana na malalamiko ya muda mrefu ya
uharibifu wa mazingira na uuaji hovyo wa wanyama wanaokatisha kwenye vijiji
hivyo wakitokea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kuelekea Mikumi.

Sheria ndogo zilizizopitishwa na wananchi kwa msaada
wa Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo –LEAT inayofadhiliwa na USAID, na kuidhinishwa na
baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa huenda zikawa mwarobaini wa malalamiko ya madiwani
yanayosababishwa na kukithiri kwa uharibifu wa mazingira.


Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Bi. Kissa Mbila amesema, "Sasa
kijiji kitakuwa na uwezo wa kusimamia sheria hizo kwa kuwaadhibu wanaoikiuka
sheria ndogo badala ya kutegemea Halmashauri na hivyo kuongeza ulinzi wa
raslimali zake".

Vijiji hivyo vinapakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na ni
miongoni mwa maeneo ambapo wanyama huvuka kwenda maeneo mengine.

LEAT inapongeza vijiji hivyo kutambua umuhimu wa uhifadhi wa maliasili zinazowazungukua na kufikia lengo la kuweza kupitisha sheria ndogo hizo. Pia inatambua mchango wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa kwa kuidhinisha sheria ndogo hizo lakini pia mwandishi kutoka Televisheni ya Taifa TBC1 Bi Irene Mwakalinga kwa kuripoti taarifa hii.