Mafunzo hayo ni njia moja wapo ya kurahisisha utekelezaji wa mradi wa Ushiriki wa wananchi katika Usimamizi wa Maliasili. Mradi huo umefadhiliwa kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia shirika la maendeleo la watu wa marekani(USAID). Huu ni mradi wa miaka minne, ulianza kutekelezwa mwaka 2014 unatarajiwa kukamilika mwaka 2017.
Lengo la mradi huu ni kuwajengea uwezo wananchi iliwaweze kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa maliasili (misitu na wanyama pori) kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya.
Mpaka sasa LEAT imewajengea uwezo takriban wadau 1500, ikiwa ni pamoja na wananchi wa kawaida, viongozi wa vijiji, kakamati za ardhi, kamati za maliasili za vijiji na wilaya.
Wadau wa utekelezaji wa mradi walio jengewa uwezo ni kutoka Iringa vijijini ni taasisi za MBOMIPA na MJUMIKK na Mufindi walikuwa ASH-TECH na MUVIMA.
Thomas Mtelega, Afisa Programu wa ASH-TECH akiwasilisha mapango kazi wa taasisi yao
Afisa Mradi wa LEAT, Musa Msanizu (katikati) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa ASH-TECH Erasto Mazela (kulia) na Afisa Programu wa ASH-TECH, Thomas Mtelega
Afisa Mradi Mwandamizi wa LEAT, Remmy Lema akimwelekeza Afisa Mradi wa MUVIMA, Winnie Moses namna ya kutengeneza bajeti ya mradi
No comments:
Post a Comment