Tarehe 28 Aprili 2014 ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa Chama cha wanasheria watetezi wa mazingira(LEAT) kwani ilifikisha miaka ishirini wa uhai wa taasisi hii. Imekuwa ni miaka 20 ya huduma kwa watanzania na mazingira yao.Imewezesha wanasheria-mazingira kushirikiana na wanasheria wengine ndani na nje ya nchiyetu kupambana na uharibifu wa mazingira, kukuza uelewawa sheria za mazingira katika nchi yetu na kutoa msaada wa klisheria kwa waathirika wa uharibifu wa mazingira. Kuanzishwa kwa LEAT mnamo miaka 20 iliyopita. kilikuwa kitu cha aina yake kwani LEAT ndiyo asasi ya kwanza ya wanasheria yenye kutetea utunzwaji na ulundwaji wa mazingira kwa maslahi ya jamii na nchi kuanzishwa Tanzania. LEAT ilipoanzishwa ilikumbana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa sheria mama ya mazingira nchini, kutokuwepokwa taasisi ya kiserikali yenye jukumu la mwisho katika utunzwaji wa mazingiranchini. Mazingira yalitunzwa kwa mazoea na si kwa sheria ukiondoa maeneo ya hifadhi za kitaifa za misitu na wanyamapori. Katika kipindi cha miaka 20 mengi yamebadilikana mengine bado hayajabadilika. Hivi sasa nchi yetu ina Sheria mwongozo ya mazingira, na Baraza la Usimamizi wa mazingira(NEMC). Hiyo ni hatua kubwa na ambacho hakijabadilika ni uchafuzi wa mazingira. Licha ya kutungwa kwa sheria ya mazingira na NEMC bado utunzaji wetu wa wa mazingira ni mbaya.Makazi yetu mengi ni machafu,Nyumba zinajengwa bila kufuata na kuheshimu kanuni za mipango miji na matumizi ya ardhi. Kibaya zaidi ni kuwa taasisi za kiserikali za mazingirazimekuwa zikifanya usimamizi wa mazingira kwa njia ya kushikizia. Miaka 20 ya LEAT imekuwa na changamoto zake ikiwa ni pamoja kutokukubalika kwa yale inayoyapigania katika baadhi ya taasisi za serikali na makampuni binafsi. Kwa mfano kampeni zake za kupigania haki za wachimbaji wadogo wa Bulyanhulu haikupokelewa vizuri na serikali kitu ambacho kilisababisha baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa LEAT kuweka ndani na kufunguliwa kesi ya uchochezi. Aidha LEAT nusura ifutiwe usajili wake. Changamoto hizi zilisababisha LEAT kubadili muundo wake na kuwa kampuni isiyon na hisa na hivyo kupata kinga ya kisheria.Ufutwaji wake unaweza kutokea tu kama wanachama wataamua hivyo au kufutwa na mahakama baada ya taratibu zote za kuendeshwa kesi kufuatwa. Changamoto nyingine ni Rasilimali watu na pesa. LEAT imekumbana na changamoto hii ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa katika kutoa huduma huduma zake kwa watu wengi. LEAT Inapenda kutoa rai wa wafadhili mbalimbali ndani na nje ya nchi kuiunga mkono LEATkwa kutoa ufadhili utakaoiwezesha kufanya mambo mengi makubwa katika nchi yetu. LEAT inapenda kuwashukuru wafadhili wote ambao wameiunga mkono kwa kipindi chote ca miaka 20 ya uhai wake. Ufadhili wao umeiwezesha LEAT kufanya tafiti muhimu za Sheria -mazingira, Sera za maliasili na mazingira, madini,misitu,wanyamapori,na mabadiliko ya mfumo-hewa na majira kwa upande mmoja na kuweza kutoa msaada wa kisheriakwa jamii mbalimbali hapa nchini.Umewezesha wafanyakazi wake kupata mafunzo mengi ya masuala ya kisheria na mazingira ikiwa ni pamoja na shahada za uzamili. LEAT inawahakikishia wafadhili kuwa inathamini sana ufadhili wao na itahakikisha kuwa inatumia ufadhili na ruzuku kutoka kwao kukuza na kuendeleza maslahi ya umma.
No comments:
Post a Comment