Timu ya Wanasheria
Watetezi wa Mazingira (LEAT) inafanya programu ya kuiwezesha jamii kutunza
Mazingira na kuibua miradi kupitia Mbinu Shirikishi ya Kujifunza kwa Vitendo
(Participatory Learning and Action/People Owned Process) ambayo inasimamiwa na
Asasi iitwayo Mtandao wa mazingira Tanzania
(Mazingira Network Tanzania (MANET) iliyopo Morogoro na kufadhiliwa na Mfuko wa dunia wa wanyamapori (WWF-Norway.)
MANET inafanya programu hii kwa kushirikisha Asasi mbalimbali Tanzania kwa
lengo la kuwezesha jamii zote kuibua na kumiliki miradi yao wenyewe pasipo
kutegemea wawekezaji au Wafadhili). MANET iliweza kuteua wakala wa mabadiliko
(Young Environmentalist Trainee (YET)) kutoka kila asasi nchini Tanzania.
Kutoka LEAT Bi Edina Tibaijuka ambaye ni Afisa Mazingira na mkuu wa Idara ya udhubiti wa taka na uchafuzi wa Mazingira. aliteuliwa
kuwa wakala wa mabadiliko(YET) na
kuiwakilisha asasi kwenda kupata mafunzo hayo ya PLA/POP.
Katika harakati za
kuendeleza mradi huu LEAT iliamua kutoa mafunzo haya katika kitongoji cha
Majani Mapana wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani kwasababu ni moja ya wilaya
inayokumbana na changamoto ya uchafuzi wa Mazingira uliosababishwa na uwepo wa
dampo katikati ya makazi ya wanajamii hao. Hivyo hali hii inazidi kurudisha
nyuma hali ya utunzaji Mazingira na hali ya uchumi kwa jamii ya watu wa Majani
Mapana.
Hivyo tangu mwezi
Oktoba 2013 hadi hivi sasa LEAT imekuwa ikishirikiana kwa ukaribu na wanajamii
wa Majani Mapana katika kutoa mafunzo ya elimu shirikishi ya kujifunza kwa
vitendo (PLA/POP) ili kuhakikisha wanajamii wanaweza kutatua changamoto
mbalimbali za Mazingira na kuweza kubadilisha mitazamo yao juu ya utegemezi.
LEAT inaamini ifikapo mwisho wa mwaka huu ambapo ndio utakuwa mwisho wa
programu hii Jamii hii itaweza kujisimamia yenyewe katika kulinda Mazingira na
kuendeleza miradi mbalimbali ya utunzaji Mazingira.
No comments:
Post a Comment