Timu ya wanasheria watetezi wa mazingira (LEAT) kupitia mradi wa
Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili ( CEGO-NRM) ambao upo chini
ya Ufadhili wa Shirika la maendeleo la misaada la watu wa Marekani (USAID)
inaendesha mafunzo ya Usimamizi wa Maliasili kwa kupitia dhana ya mfumo wa
Ufuatiliaji wa Uwajibikaji jamii
(UJJ/SAM) katika mkoa wa Iringa,
wilaya mbili za Iringa vijijini na Mafinga.
Mafunzo yalianza mnamo mwezi wa nane na yataendelea hadi mwezi wa kumi
mwaka 2014. Walengwa wakuu wa mafunzo haya ni Kamati za Mazingira za vijiji
kama vile kamati za maliasili, kamati za maji, kamati za matumizi bora ya
ardhi, kamati za mipango na fedha, baraza la ardhi na kamati nyingine
zinazohusika na mazingira vijijini.
Hadi sasa LEAT imeweza kuzifikia
kamati hizi na kuwapatia mafunzo ambapo mpaka sasa Katika wilaya ya Iringa
vijijini LEAT imeweza kuifikia kata ya KIwere na Idodi ambapo katika kata ya Kiwere wkamati za mazingira za
vijiji vya kiwere, Mfyome,Kitapilimwa na itagutwa vimenufaika na mafunzo haya,
vilevile katika kata ya Idodi kamati za vijiji za Tungamalenga, idodi
zimefikiwa na kuelimishwa wakati kijiji cha Kitisi kikitegemea kufikiwa na
Mafunzo haya mwanzoni mwa mwezi wa kumi.
Kadhalika katika wilaya ya Mafinga LEAT imekusudia kuzifikia kata Mbili
ambazo ni Igombavanu na Saadani ambapo mpaka sasa LEAT imeweza kuvifikia vijiji
vya Igombavanu, uhambila Lugoda lutali na Tambalang’ombe katika kata ya
igombavanu wakati katika kata ya Saadani LEAT imeweza kuvifikia vijiji vya
Kibada,Mapogolo wakati kijiji cha utosi kikitegemea kufikiwa mwanzoni mwa mwezi
wa kumi.
Mafunzo haya yamelenga kuwafikia angalau wajumbe 35 wa kamati za
Mazingira kwa kila kijiji na lengo kuu la mafunzo haya ni
I. Ni kuijengea uwezo jamii kufahamu mwelekeo sahihi
wa uwajibikaji jamii.
II. Kuelewa dhana ya mfumo
wa uwajibikaji jamii katika usimamizi wa misitu na wanyamapori.
III. Pia kuelewa hatua
tano za mchakato wa mfumo wa uwajibikaji jamii ikwa ni pamoja na mpango wa
mgawanyo wa rasilimali, usimamizi wa matumizi, usimamizi wa uadilifu na
usimamizi wa uangalizi.
Vilevile mafunzo ya ufuatiliaji na
usimamizi wa uwajibikaji wa jamii yanalenga kuongeza uelewa juu ya zana za
uwajibikaji na usimamizi wa jamii kwa kufuatilia kila hatua ya mchakato.
Hivyo basi ufualiaji wa uwajibikaji jamii
unawezesha watoa huduma kwa jamii kutoa ufafanuzi, uthibitisho na uhalalisho
juu ya mgawanyo wa raslimali za umma, utekelezaji wake na ufanisi/utendaji
wake. Lengo ni kuhakikisha kuwa viongozi wa serikali pamoja na watoa huduma
wote wanawajibika na wanawajibishwa ipasavyo pale wanaposhindwa kufikisha
huduma muhimu kwa jamii kama walivyoorodhesha katika mpango mkakati, Mpango
mwaka na bajeti ya Mwaka ili kuweza kufikia haki za msingi za
binadamu/mwananchi.
No comments:
Post a Comment