Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) imefanya
tathmini kwa Asasi nne ili kupima kiwango cha uchechemuzi (ushawishi) cha Asasi
hizo ambazo ni washirika wa utekelezaji wa mradi wa ‘Ushiriki wa Wananchi
katika Usimamizi wa Maliasili’ unaotekelezwa katika vijiji 32 vya wilaya za
Iringa na Mufindi Mkoani Iringa, kwa ufadhili wa Watu wa Marekani. Tathmini
ilifanyika mwishoni mwa mwezi Juni, 2016 kwa Asasi za ASH-TECH na MUVIMA za
Wilaya ya Mufindi; na kwa Wilaya ya Iringa ni MBOMIPA na MJUMIKK.
Tathmini hiyo ili lenga kuangalia iwapo agenda za
uchechemuzi zimepewa kipaumbele ili kufikia malengo ya mradi, pia kuangalia endapo
mipango hiyo imehusisha mambo muhimu ikiwa ni pamoja na kujumuisha wanawake na
makundi yenye mahitaji maalum; ili kuyafikia makundi yote katika jamii.
Zaidi tathmini hiyo
ili lenga kubaini endapo wadau wa utekelezaji uchechemuzi ikiwa ni pamoja na
wafanyakazi na bodi za Asasi, wananchi na taasisi washirika wanafahamu na wanashiriki
katika uainishaji na utekelezaji wa agenda za uchechemuzi.
Hatua hiyo ni muhimu kwa LEAT na Asasi hizo kwa kuwa mafanikio
ya mradi yana changiwa na utekelezaji thabiti wa mipango ya uchechemuzi ambayo
hutumika kutatua changamoto zinazo ikabili sekta za misitu na wanyamapori, kwa kutumia
njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na kushinikiza wafanyamaamuzi kuchukua hatua
juu ya changamoto hizo.
Kutoka kulia, Afisa Mradi wa LEAT, Musa Mnasizu; Mjumbe wa MJUMIKK,Mchungaji Ombeni; Ktibu Muu wa MJUMIKK, Mashaka Kilanga an Mratibu wa MJUMIKK, Simon Komba
Kutoka kushoto: Afisa Mradi wa MUVIMA,Winnie Moses; Mkurugenzi Msaidizi wa MUVIMA, Speratus Mbeyela; Mkurugenzi- MUVIMA, Albert Chalamila; na Afisa Mradi wa LEAT- Jamal Juma
Baada ya siku sita za tathmini ya uchechemuzi, LEAT pamoja
na Asasi waliainisha mapungufu yaliyoonekana katika mikakati ya uchechemuzi, na
walipendekeza njia za kuboresha.
LEAT ili jengewa uwezo na Mtaalamu wa Uchechemuzi Tobias
Chelechele kutoka Shirika la Pamoja Twajenga, ambao ni wakala wa Shirika la
Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID). Mradi wa ‘Ushiriki wa Wananchi
katika Usimamizi wa Maliasili’ unahusu rasilimali misitu na wanyamapori.
Takriban wananchi 6500 watanufaika na mradi huo. Mradi
unatoa mafunzo ya usimamizi wa misitu, wanyamapori na ufuatiliaji uwajibikaji
jamii, ili kuzijengea uwezo jamii kusimamia, kulinda na kuhoji viongozi
waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali misitu na wanyamapori. Ili kufikia wananchi
wengi, LEAT inaendelea kutoa elimu kwa njia ya Sanaa kupitia vikundi viwili vya
Sanaa, makala za magazeti na programu za vipindi vya redio. Kwa kuwa mradi
umelenga kujenga misingi ya utawala bora katika sekta ya misitu na wanyamapori,
LEAT inatoa mafunzo kwa viongozi wa Vijiji, Madiwani, Wananchi, Maafisa misitu
na wanyamapori.