Na, Heri Ayubu
FRIENDS OF THE EARTH, TANZANIA.
Mnamo May 17, Kampuni ya BARRICK GOLD ilitoa tamko rasmi la kukubali mauaji ya watu 5 na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa katika eneo la mgodi. Mauaji yametokea chini ya mikono ya polisi, ambao kwa mujibu wa Barrick walikuja kuwasaidia kutokana na waliowaita ‘wavamizi zaidi ya 800’ ambao walitaka kuingia eneo mgodi kwa nguvu kwa lengo la kuiba mchanga wa dhahabu. Tangu tikio hili itokee kumekuwa na migogoro mikubwa katika eneo hilo, na kushuhudiwa kuongezeka kwa idadi ya polisi, machafuko na zaidi kutiwa nguvuni kwa Wabunge wawili, akiwemo Mhe. Tundu Lissu; waandishi wa habari wane; mwanasheria wa CHAMA CHA WANASHERIA WATETEZI WA MAZINGIRA- LEAT, Bwana Stanslaus Nyembea, pamoja na mwananchi mmoja.
Mhe. Tundu Lissu (Mbunge) |

Mgogoro na mauaji ya aina hii sio kitu kigeni, kwani mnamo mwaka 2010, mwandishi wa Habari wa shirika la Bloomberg, Cam Simpson alilipoti kuwa watu saba (7) waliuawa katika mgogoro huo na askali wa ulinzi wa BARRICK wakishirikiana na askali polisi (wanaolipwa na Barrick) katika mgogoro kama huu. Hivyo unapozungumzia ulinzi wa mgodi wa Barrick unajumuisha Jeshi la polisi pamoja na walinzi binafsi wa mgodi.
Mfumo wa utawala wa Sheria wa Tanzania unafahamika, ya kwamba ni MAHAKAMA pekee ndicho chombo chenye Mamlaka kisheria ya kumhukumu mtu kama Mkosaji na kumpa adhabu stahili. Kabla ya hapo mtu anayedhaniwa ni mharifu ni mtuhumiwa tu anayetakiwa kufikishwa kwenye mamlaka husika. Hili linamshangaza Mhe. Machage Bartholomew ambaye ni mjumbe wa Baraza la Wilaya alipohojiwa na mwandishi Simpson. “wanawapiga tu risasi, hawatii nguvuni na kuwafikisha mahakamani” alisema Mhe. Machage.
Historia ya mvutano huu inaweza kutazamwa kutoka kwenye matatizo ya uhamishwaji wa wakazi wa eneo la mgodi kupisha uwekezaji, pamoja na kunyang’anywa maeneo yao waliyokuwa wakifanya shughuli za uchimbaji mdogo (SMALL SCALE MINING). Kabla ya ‘uwekezaji’ wa wageni, eneo hilo lilikuwa na wachimbaji wadogo wasiopungua 40,000 (elfu arobaini) waliokuwa wakiendesha maisha yao kwa shughuli za uchimbaji wa madini. Wachimbaji hawa wadogo wanafanya jumla ya vijiji vitano (5) vilivyokuwa na HAKI ya kumiliki ardhi ya eneo la mgodi, LAKINI waliondolewa katika eneo lao kwa NGUVU na kinyume na taratibu na eneo kupewa iliyokuwa ikijulikana kama AFRIKA MASHARIKI GOLD MINES LTD, hii ni kwa mujibu wa kesi ililowasilishwa Julai 2003 na CHAMA CHA WANASHERIA WATETEZI WA MAZINGIRA (LEAT) ikiwawakilisha waliokuwa wachimbaji wadogo wapatao 1273. Katika kesi nyingine wamiliki wa ardhi zaidi ya 43 walidai kutolipwa fidia yoyote baada ya kuondolewa kwa nguvu kwenye maeneo yao.
Tangu wakati huo kumekuwa na migogoro isiyokwisha katika eneo hilo. Mnamo mwaka 2008 tukio moja la wananchi kudai haki zao lilipelekea kuchomwa moto kwa mali za kampuni zenye thamani ya Dola za kimarekani Million Saba ($ 7,000,000/-). Kwa mara nyingine BARRICK walitupa lawama kwa walivyoviita ‘vikundi vilivyojipanga’ kuvamia eneo lao. Mwezi mmoja baadae mwanakijiji mwingine alikufa mikononi mwa walinzi wa BARRICK. Hivyo migogoro na mauaji haya kwa makazi wa Tarime sio kitu kigeni kabisa, kwa mujibu wao imekuwa iktokea mara kwa mara na kumekuwa na tabia ya kuwaua kwa kuwaita wezi.
Pia jamii isisahau hata kidogo kile kilichotokea mwaka 2009, ambapo kemicali-sumu aina ya CYANIDE ilivuja na kuchanganyikana na maji yam to THIGITE, mto unaotumiwa na wanakijiji wa Nyamongo kama chanzo kikuu cha maji ya matumizi ya kila siku. Kutokana na tukio hilo, inakadiriwa watu wapatao Arobaini (40) walipoteza maisha, mamia wakiachwa na ulemavu wa kudumu na mifugo zaidi ya Mia Tano (500) ilikufa kutokana na kutumia maji yaliyochanganyikana na kemikali hiyo yenye sumu. Huzuni na Majonzi makubwa vimmeendelea kuwa mioyoni mwa Wakazi hawa na kuzaa Chuki na Hasira kubwa juu ya kampuni hii ya kigeni. Pia kuna kundi kubwa limeachwa halijiwezi baada ya kuathiriwa vibaya na maji hayo.
Kufuatia tukio hilo, Kitu cha kusikitisha ni wananchi walioathirika ndio waliotuhumiwa kuiba kapeti iliyokuwa chini ya ardhi (underground protective carpet) na kusababisha kuvuja kwa kemikali-sumu. Tuhuma hiyo, pamoja na kutaka kuwaweka hatiani wanakijiji wa kile kilichowaathiri wao wenyewe na kutaka kuisafisha kampuni ya AFRICAN BARRICK, imewanyima WAATHIRIKA HAWA hata haki yao ya kupata fidia kutokana na madhara waliyopata. Zaidi ya kuathirika kwa binadamu na mifugo mazingira kwa ujumla yaliathirika kwa kiasi kikubwa, na kuathiri rutuba na uwezo wa uzalishaji wa ardhi ambayo wanakijiji huitegemea kwa uhai wao.

“Unaweza ukapata picha ni hali gani waliyonayo wanakijiji hawa kwa maisha yao, baada ya yote hayo, wamekata tamaa na maisha……. Madini kuwa katika eneo lao imekuwa ni kama laana kwao…… selikali haipo upande wao tena bal indo hivi polisi na walinzi wanashirikiana kuwaua watoto wao na wanakijiji wenzao…… inasikitisha sana” Alisema mmoja wa waliohojiwa kwa masharti ya kutokaririwa.
Tukirudi kwenye mauaji ya hivi majuzi, kilichowashangaza wengi ni kitendo cha polisi ‘kuvamia’ chumba cha kuhifadhia miili wa marehemu (mortuary) na kuiba miili mine, kwa lengo la kuzuia wanakijiji kufanya maziko ya kumbukumbu ya pamoja yaliyopangwa kufanyika Jumanne ya tarehe 17th May 2011. Hii ni kwa mujibu wa wanakijiji wa Nyamongo huko Tarime.